Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela, ameahidi kufanya Maboresho makubwa katika Miundombinu ya Viwanja vya Ndege Tanzania na katika kuhamasisha kasi ya utendaji ya wafanyakazi katika Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania.

Hayo ameyazungumza mbele ya Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe katika mkutano na waandishi wa habari baada ya kufanya ukaguzi wa miundombinu katika jengo la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).

Awali Waziri Kamwelwe alianzia ziara yake Katika Kiwanja cha Ndege cha Songwe na kubaini kwamba njia ya kuruka na kutua ndege imejegwa chini ya kiwango na mkandarasi lakini pia alipotua JNIA alibaini pia baadhi ya changamoto.

Kufuatia hatua hiyo Waziri Kamwelwe ametoa maagizo kwa TAA kwamba kuanzia Januari mwakani kuwe na mabadiliko katika namna ya utendaji.
“Nawaomba ndugu zangu kuanzia Januari mwakani mbadilike na kama mtu hata badilika basi tutamtoa. Malalamiko ya watu mimi nayapokea na ninayafanyia kazi, kwa maana hiyo ni vyema pia muyafanyie kazi”, alisema Mhandisi Kamwelwe.  
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela akimweleza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (kulia), changamoto zinazoikabili Mamlaka hiyo, wakati alipotembelea kukagua miundombinu mbalimbali kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).

2-min
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza na Menejimenti na Waandishi wa Habari baada ya kufanya ziara ya kukagua miundombinu ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela.
3-min
Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (kulia) jana akizungumza na Wafanyakazi wa Kampuni ya inayotoa huduma kwa abiria na mizigo ya Swissport Tanzania, Bi. Sarah Mlawa (kushoto) na Fliora Temba, alipokuwa akikagua miundombinu ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
4-min
Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (kulia) akimsikiliza Msimamizi Kitengo cha Mitambo, Bw. Gregory Kosamu (wa pili kushoto) aliyekuwa akielezea mifumo ya Kiyoyozi ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA). Watatu kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Roichard Mayongela na kushoto ni Kaimu Meneja Matengenezo na Huduma za Kiufundi, Bi. Diana Munubi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...