Na Mathias Canal, Songwe
Serikali imesema hakuna kijiji nchini kitakachoachwa bila ya kuunganishiwa umeme katika awamu ya tatu ya mradi unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (Rea).
Aidha, Serikali imetenga Sh1 trilioni kwa ajili ya kusambaza umeme katika vijiji 8,000 ambavyo bado havijaunganishiwa na nishati hiyo huku ikiendela na uwekaji wa umeme katika vijiji zaidi ya 13400.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe Mhe Japhet Hasunga amewahakikishia wananchi kuhusu upatikanaji wa umeme katika jimbo hilo hivyo wananchi wanapaswa kuondoa wasiwasi na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli.
Mhe Hasunga ameyasema hayo wakati wa mikutano yake katika kijiji cha Igale na Iyula A vilivyopo katika kata ya Iyula akiwa katika ziara ya kikazi jimboni humo iliyoanza juzi tarehe 22 Octoba 2018.Alisema kuwa upatikanaji wa umeme katika jimbo lake utasaidia kuongeza upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii na kuwa chachu ya maendeleo kwa wananchi na Taifa kwa ujumla wake.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo kuhusu upatikanaji wa umeme katika jimbo la Vwawa wakati akiwa katika ziara ya kikazi jimboni kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi. (Picha Zote Na Mathias Canal)
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo kuhusu upatikanaji wa umeme katika jimbo la Vwawa wakati akiwa katika ziara ya kikazi jimboni kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Baadhi ya wananchi wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe wakifatilia mkutano wa Mbunge wa jimbo hilo ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga wakati akiwa katika ziara ya kikazi jimboni kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...