NA MWAMVUA MWINYI, KISARAWE
MBUNGE wa viti maalum mkoani Pwani, Zainab Vullu ametoa msaada wa mapazia mazito yanayotumika kusaidia kuweka usiri kwa akinamama wanaokwenda kujifungua katika wodi ya uzazi hospital ya wilaya ya Kisarawe.
Msaada huo unaelezwa kuwaondolea kero waliyokuwa wakiipata akinamama hao kipindi cha nyuma ambapo walikuwa wakikataa kujifungua hospitalini hapo kwa kuhofia kukosa faragha wakati wa kujifungua.
Mbali ya msaada huo pia ametoa mifuko 80 ya saruji kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya ,zahanati na shule vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya sh.milioni mbili.
Akitoa msaada huo ,Zainab alieleza kipindi cha nyuma akinamama wanaojifungua walikuwa wanakaa sehemu ambayo haijazibwa jambo ambalo limemsukuma kujitolea mapazia hayo. “Faragha inaanza tangu pale anapoanza kutafutwa mtoto hadi anapozaliwa lazima usiri uwepo,” alifafanua Zainab.
Nae mkuu wa wilaya ya Kisarawe ,Jokate Mwegelo alimshukuru mbunge huyo na kudai suala la ukosefu wa mapazia hayo ilikuwa ni changamoto kwa akinamama wanaojifungua.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Hamis Dikupatile alisema, serikali imekuwa ikijitahidi kuboresha mazingira ya kutolea huduma lakini bado jitihada zinapaswa kufanywa na kila mmoja. Mganga mkuu wa halmashauri ya Kisarawe, Jonathan Budenu alibainisha kutokana na changamoto hiyo baadhi ya akinamama walikuwa wakikataa kujifungulia hapo kutokana na hali hiyo.

MBUNGE wa viti maalum mkoani Pwani, Zainab Vullu akikata utepe,kulia ni MKuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...