Na Stella Kalinga, Simiyu 

Wadau mbalimbali wa elimu wamechangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Halmashauri ya Wilaya ya Busega mkoani Simiyu katika Harambee iliyofanyika Mjini Nyashimo, ambapo zimepatikana jumla ya shilingi 254, 969,000/= fedha taslimu zikiwa ni shilingi 15,360,000/= ahadi shilingi 241,809,000/= na mifuko ya saruji 127.

Akiongea na wadau hao Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo ambaye alialikwa kama Mgeni rasmi wa Harambee hiyo, Luteni Kanali Josephat Mshashi, Mkuu wa Kikosi cha 27 Makoko Musoma amesema upo umuhimu wa kuhakikisha watoto wanapata elimu kwa kuwa elimu ni urithi hivyo kila mmoja awe na uchungu wa kuona watoto wanasoma. 


“Hakuna urithi tunaoweza kuwapa watoto wetu zaidi ya elimu tusipowapa elimu rasilimali zote ambazo tunazipigania leo hii, tunavyopambana kulikomboa Taifa letu kiuchumi itakuwa kazi bure kwa sababu tutabaki na Taifa la watu ambao ni watumwa wa watu wenye elimu” alisema Mshashi

Awali akitoa taarifa ya hali ya vyumba vya madarasa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Bw. Anderson Njinginya amesema halmashauri hiyo ina upungufu wa vyumba vya madarasa 107.

Mmoja wa Wadau wa elimu katika Wilaya ya Busega, Bw. Deo Kumalija ambaye alichangia katika harambee hiyo ametoa wito wadau wa maendeleo na wananchi kuchangia shughuli za maendeleo katika maeneo waliyopo, ikiwemo ujenzi wa shule kwa kuwa maendeleo yao yataletwa na wao wenyewe.
Wadau wa elimu na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Simiyu wakichangia katika harambee ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa wilayani Busega, iliyofanyika Mjini Nyashimo lengo likiwa ni kukabiliana na changamoto ya vyumba vya madarasa wilayani humo. 

Wadau wa elimu na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Simiyu wakichangia katika harambee ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa wilayani Busega, iliyofanyika Mjini Nyashimo lengo likiwa ni kukabiliana na changamoto ya vyumba vya madarasa wilayani humo. 
Mkuu wa Wilayaya Busega Mhe. Tano Mwera (kushoto) na Mbunge wa Busega,Mhe. Dkt. Raphael Chegeni wakiteta jambo katika harambee ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa wilayani Busega, iliyofanyika Mjini Nyashimo lengo likiwa ni kukabiliana na changamoto ya vyumba vya madarasa wilayani humo. 
Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo ambaye alialikwa  kama Mgeni rasmi wa Harambee hiyo, Luteni Kanali Josephat Mshashi, Mkuu wa Kikosi cha 27 Makoko Musoma akizungumza na wadau wa elimu, katika harambee ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa wilayani Busega, iliyofanyika Mjini Nyashimo lengo likiwa ni kukabiliana na changamoto ya vyumba vya madarasa wilayani humo.  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...