Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo ametaja majina nane ya wanachama ya Yanga wanaodaiwa kuwakwamisha uchaguzi wa Yanga ambao umepangwa kufanyika Januari 13.

Akitoa taarifa kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harisson Mwakyembe, Singo amesema kuwa Waziri alipokea majina ya watu wanaosababisha kukwamishwa kwa uchaguzi huo na wamekuwa wanafanya vikao vingi vya siri ili kuhakikisha haufanyiki.

Amesema, majina hayo yamefikiwa kwa Waziri na raia wanaopenda soka liende mbali na liwe na maendeleo na tayari majina hayo yamepelekwa kwenye vyombo vya usalama ili wafanye uchunguzi na wakibainika wachukuliwe hatua.

"Waziri umeyachukua majina hayo na kuyapeleka katika vyombo husika vya serikali na kama watabainika ni kweli hatua kali zitachukuliwa dhidi yao," amesema Simgo.Singo amesisitiza kuwa, tayari kauli ya mwisho ya Serikali wameshaitoa ya Uchaguzi wa Yanga ufanyike Januari 13 sasa wanachama hawa wanakuwa wanapinga suala hilo wakidai kuwa hawautambui uchaguzi huo kutokana na kusimamiwa na Shirikisho la Mpira Nchini (TFF) na wakisisistiza kuendelea kumtambua aliyekuwa Mwenyekiti wao Yusuf Manji.

Majina ya watu hao yaliyowekwa hadhani ni pamoja Mustapha Mohammed, Edwin Kaisi, Said Bakari, Shaban Omary, Kitwana Kondo, Boazi Ikupilika, Bakiri Makere na David Sanare.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...