Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge amewataka watendaji
wa Mkoa wa Dodoma kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili kujenga
mazingira rafiki na kuboresha mazingira ya biashara.
Ametoa
kauli hiyo leo wakati akifungua kikao kazi cha siku moja cha
Baraza La Biashara Mkoa wa Dodoma kilicholenga kujadili Mwongozo wa
Uwekezaji mkoani humo Desemba 21, 2018 katika Chuo cha
Mipango.Dkt.Mahenge aliwataka watendaji kuzingatia utendaji wenye
weledi,
tija na unaovutia wawekezaji kuwekeza mkoani humo kwa kuzingatia kuwa
ndiyo Makao Makuu ya Nchi.“lazima utendaji wetu uwe wa namna bora na upekee katika kuweza
kuvutia wawekezaji kwa kuwa na miundombinu rafiki ya biashara na kutatua
changamoto zozote zinazoweza kuwakwamisha wawekezaji”.Alieleza
Dkt.Mahenge.
Aliongeza kuwa, Halmashauri zote zione umuhimu wa kuboresho
mazingira ya uwekezaji na kutumia fursa zilizopo katika kufikia malengo
ya kujenga uchumi endelevu.“Nivyema sasa kila Halmashauri ikaona fursa na kuzitumia ikiwemo zile
za kifedha na kuhusisha taasisi za kifedha ikiwemo Mabenki ili kuona
kila lengo linafikiwa na kuwa na uwekezaji wenye tija
nchini”.alisisitiza Dkt.Mahenge
Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Bw. Godwin Kunambi alieleza umuhimu
wa kuzitumia fursa zilizopo Dodoma na kuwa na uwekezaji wenye tija kwa
kila eneo kwa kuzingatia mazingira yaliyopo.
“Lazima fursa zilizopo Dodoma zitumike kwa malengo yenye tija kwa
kuhakikisha mkoa unabaki kuwa kivutio cha wawekezaji wa ndani na nje ya
nchi ,”Alieleza Kunambi.Aliongeza kuwa Jiji hilo limetenga maeneo mbalimbali ya uwekezaji na
kuyapima kulingana na mahitaji ya uwekezaji ikiwemo ya viwanda, Biashara
na makazi.Kikao kazi cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Dodoma kimefayika ili
kupitia muongozo wa uwekezaji katika mkoa wa huo hali itakayochochea
uwekezaji na kukuza uchumi na kuchochea maendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akifungua kikao kazi cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Dodoma kilicholenga kujadili na kutoa maoni kuhusu muongozo wa uwekezaji katika mkoa huo leo jijini humo.
Muwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara Bw. Patrick Mavika akizungumza wakati wa kikao kazi cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Dodoma kilicholenga kujadili na kutoa maoni kuhusu muongozo wa uwekezaji katika mkoa huo leo jijini humo.
Wajumbe wa Baraza la Biashara la mkoa wa Dodoma wakifuatilia kikao kazi cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Dodoma kilicholenga kujadili na kutoa maoni kuhusu muongozo wa uwekezaji katika mkoa huo leo jijini humo.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Bw. Godwin Kunambi akizungumzia fursa zilizopo katika Jiji Dodoma wakati wa kikao kazi cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Dodoma kilicholenga kujadili na kutoa maoni kuhusu muongozo wa uwekezaji katika mkoa huo leo jijini humo.
Mtafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Bw. Mussa Martine akiwasilisha mada wakati wa kikao kazi cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Dodoma kilicholenga kujadili na kutoa maoni kuhusu muongozo wa uwekezaji katika mkoa huo leo jijini humo.
Meya wa Jiji la Dodoma Prof. Davis Mwamfupe akizungumza wakati wa kikao kazi cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Dodoma kilicholenga kujadili na kutoa maoni kuhusu muongozo wa uwekezaji katika mkoa huo leo jijini humo.(Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...