Watumishi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA ) wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, weledi, sheria na kanuni zinazosimamia utumishi wa umma ili kufikia malengo yakutoa huduma bora kwa wananchi hasa wanyonge kama dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano inavyoelekeza.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa OSHA, Mkurugenzi wa Idara ya Vijana Bw. James Kajugusi amesema kuwa kikao hicho ni fursa pekee ya kutathmini utendaji wa wafanyakazi na kuangalia namna ya kuboresha ili kufikia malengo yaliyowekwa. “Baraza hili la Wafanyakazi linasisitiza umuhimu wa watumishi kufanya kazi kwa maadili na nidhamu ya hali ya juu kama wakaguzi wa masuala ya Afya na Usalama katika maeneo ya kazi ili muweze kuwa mfano wa kuigwa na Taasisi nyingine za Umma zinazofanya kazi zinazoshabihiana na za kwenu.”
Akifafanua Bw. Kajugusi amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kwa dhati, kuondoa uzembe, ubadhirifu pamoja na vitendo vyovyote vya rushwa mahala pa kazi, ikiwa ni pamoja na kubana matumizi yasiyo ya lazima ili kuongeza tija. Aliwaasa watumishi hao kuhakikisha kuwa wanatekeleza wajibu wao kwa kuzingatia malengo yaliyopangwa kwa wakati husika ili kuchochea maendeleo.
Mkurugenzi wa Idara ya Vijana Kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. James Kajugusi, akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Jijini Dodoma wakati wa kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA) kuhusu umuhimu wa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA), Bi. Khadija Mwenda, akimkaribisha Mkurugenzi wa Idara ya Vijana Kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. James Kajugusi, kufungua kikao cha baraza la wafanyakazi wa Wakala huo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. Andrew Massawe, Jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wa Kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA) kinachofanyika Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Vijana Kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. James Kajugusi, (wa nne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA).
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...