WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua Mkakati wa Nne wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI 2018/19 - 2022/23 ambao unatarajia kupunguza maambukizi mapya ya VVU kwa asilimia 75 ifikapo mwaka 2020 na asilimia 85 ifikapo mwaka 2023. Matokeo mengine yanayotarajiwa kufikiwa kutokana na mkakati huo ni kupungua kwa maambukizi mapya ya VVU miongoni mwa watoto kwa chini ya asilimia 5 ifikapo mwaka 2023 na chini ya asilimia 2 ifikapo mwaka 2030.

Waziri Mkuu amezindua mkakati huo leo (Jumamosi, Desemba 1, 2018) kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Kitaifa jijini Dodoma na kusema kuwa matayarisho yake yamezingatia matokeo ya mapitio ya Mkakati wa Tatu wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI 2013/14 – 2017/18. Amesema mbali na matokeo hayo pia mkakati huo utawezesha kupungua kwa vifo vinavyohusiana na ukimwi  kwa asilimia  50 ifikapo mwaka 2020 na asilimia 70 ifikapo mwaka  2023 na kupunguza unyanyapaa na ubaguzi ifikapo 2023 na kuelekea kutokomeza kabisa ifikapo mwaka 2030. 

Hata hivyo Waziri Mkuu amesema mkakati huo umewianisha na kupanga programu mbalimbali zinazosaidia mwitikio wa Taifa zikiwemo afua zinazotekelezwa kupitia mpango wa dharura wa Rais wa Marekani wa uKIMWI (PEPFAR). “Pia Mfuko wa Dunia wa kudhibiti UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria (Globa Fund) na jitihada nyingine za makubaliano ya ushirikiano baina ya nchi mbalimbali na ili kupata matokeo mazuri tunapaswa kuimarisha mawasiliano na uratibu miongoni mwa wadau wote sambamba na kufuata na kutekeleza vipaumbele vilivyoainishwa.”
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Mkakati wa Nne wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi Tanzania (2018/19 – 2022/23) katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani Kitaifa, kwenye Kiwanja cha Jamhuri jijini Dodoma, Desemba 1, 2018. Wapili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na Kulia ni Naibu Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.  Faustine Ndugulile na Kushoto, Mkurugenzi Mtendaji  wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dkt. Leonard Maboko.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha Kitabu  cha  Mkakati wa Nne wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi Tanzania (2018/19 – 2022/23)  baada ya kuzindua Mkakati huo katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani Kitaifa, kwenye Kiwanja cha Jamhuri jijini Dodoma, Desemba 1, 2018.  Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na Kulia ni Naibu Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.  Faustine Ndugulile.
 Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa  akimkabidhi Kitabu cha Mkakati wa Nne wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi Tanzania (2018/19 – 2022/23) Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa Nchini, Alvaro Rodriguez baada ya kuzindua Mkakati huo katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani Kitaifa, kwenye Kiwanja cha Jamhuri jijini Dodoma, Desemba 1, 2018. Watatu kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na Kulia ni Naibu Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile na Kushoto, Mkurugenzi Mtendaji  wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dkt. Leonard Maboko. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakipita kwa maandamano mbele ya Mgeni Rasmi, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika Kilele  cha Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani Kitaifa, kwenye Kiwanja cha Jamhuri jijini Dodoma, Desemba 1, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...