Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), limetangaza kumfungia mwanamuziki Nasibu Abdul (Diamond Platnumz) na Raymond Mwakyusa (Rayvan) kutokana na kitendo chake cha kupuuzia.
Basata imesema Diamond na Rayvan wamepuuzia na kuendelea kuutumia wimbo wa “Mwanza” maarufu kama Nyegezi katika shoo zake za Wasafi Festival na kuonesha dharau na utovu wa nidhamu kwa mamlaka zinazosimamia masuala ya sanaa nchini na uvunjifu wa maadili uliokithiri.
Katika barua iliyotolewa leo mapema, Basata wameeleza pia kuwa wamewafungia wasanii hao kutokufanya shoo ndani na nje ya nchi kwa kipindi kisichojulikana kuanzia Desemba 18 2018.
Pamoja na hayo Basata wamefuta kibali cha Tamasha la Wasafi Festival kutokana na ukiukwaji wa Sheria, Kanuni na Utaratibu katika uendeshaji wa tamasha hilo hapa nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...