Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega, amemtaka mkandarasi SUMA JKT anayejenga jengo la wizara hiyo katika Mji wa Serikali Jijini Dodoma, kuhakikisha anaendelea kuwalipa wafanyakazi wanaojenga jengo hilo kwa wakati pamoja na kuhakikisha ubora wa jengo hilo unaendana na thamani hali pesa.

Mhe. Ulega amesema hayo leo (04.01.2019) mara baada ya kufika katika mji huo uliopo Kata ya Mtumba, kwa ajili ya kufanya tathmini ya maendeleo ya ujenzi wa jengo la awali la Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kuonesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi inavyoendelea na kumtaka mkandarasi kukamilisha ujenzi huo kwa wakati.

“Unamlipa mtu kabla jasho lake halijakauka palepale unakuwa tayari umeshampa ndiyo dini inavyosema, ni jambo jema sana maana hawa mafundi wanasema wanalipwa kwa wakati, sisi muda wowote tutakuwa tunakuja hapa tunataka hii kazi imalizike kwa wakati na kwa viwango” Amesema Mhe. Ulega.

Mhe. Ulega amefafanua kuwa siyo jambo jema endapo kutatokea taarifa mara baada ya kumalizika kwa mradi wa ujenzi wa jengo la Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kuwa wafanyakazi waliokuwa wakijenga jengo hilo wanamdai mkandarasi ilhali wizara imemlipa pesa zote mkandarasi huyo SUMA JKT ili aweze kufanya kazi kwa wakati.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akipewa maelezo ya ujenzi wa jengo la wizara na Mkandarasi Msimamizi wa SUMA JKT Injinia David Pallangyo, katika Mji wa Serikali Jijini Dodoma
Baadhi ya wafanyakazi wanaojenga jengo la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Mji wa Serikali Jijini Dodoma wakiendelea na hatua mbalimbali za ujenzi wa jengo hilo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...