Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii
Naibu
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amemtaka Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo, Prof. Kitila Mkumbo kuitisha haraka Mkutano kwa Wadau wote
wanaohusika na Mradi wa Maji Chalinze Jumanne ya Januari 29, mkutano
utakaojadili changamoto za upatikanaji Maji katika Halmashauri hiyo.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari baada yakutembelea Mradi huo katika eneo la
Chalinze, Mhe. Aweso amesema mpaka sasa mradi huo umefika asilimia 78 na
Serikali imewekeza zaidi ya Shilingi Bilioni 95 kuhakikisha Wananchi wa
Chalinze wanapata Maji yakutosha.
Katika
ziara yake hiyo, Mhe. Aweso amesema ameona changamoto katika uendeshaji
wa mradi huo ikiwemo vituo vya Maji zaidi ya 200 lakini 86 ndio
vinafanya kazi ya utoaji huduma ya Maji pamoja na changamoto ya
uendeshaji ikiwa sambamba nakuwapa Watoto wadogo kusimamia vituo hiyo.
Mhe.
Aweso amewata Watendaji wa Wizara hiyo kuhakikisha wanatafuta
Wakandarasi wenye weledi na kazi zao ili kuhakikisha miradi hiyo
inasimamiwa ipasavyo bila kusuasua licha ya mradi huo kufika asilimia
78.
"Mkandarasi
anayesimamia mradi huu ni changomoto, hatuwezi kumuachia mpaka amalize
mradi huu, tayari amechukua fedha zaidi ya asilimia 62 kwenye Bilioni
95", amesema Aweso
Kwa
upande wake, Msimamizi wa Mradi wa Maji, Chalinze - DAWASA, Mhandisi
Modesta Mushi amesema kuwa mradi huo umefika jumla ya asilimia 78 pamoja
na ujenzi wa Miundombinu eneo la mtambo, ujenzi wa matenki kufikisha
Maji maeneo tofauti na ujenzi wa vitekeo Maji (Viosk) jumla ya 351
maeneo mbalimbali katika eneo la mradi.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Bi. Zainabu Kawawa ameshukuru kuona ziara
ya Naibu Waziri wilayani humo, amesema wataendelea kusimamia kuhakikisha
Mkandarasi wa Mradi wa Maji, Chalinze anamaliza mradi huo kwa wakati
licha kuahidi kumaliza Desemba 31, 2018, amesema wanahitaji kuona
usimamizi mzuri katika Vitekeo Maji vilivyopo ili kutoa fursa kwa
Wananchi wa Chalinze kupata huduma hiyo ya Maji Safi na Salama.
Utekelezaji
wa Mradi huo wa Chalinze, awamu ya tatu unatekelezwa na Mkandarasi
Overseas Infrastructure Alliance (India) Private Limited pamoja na
Kampuni ya Platiba kwa gharama ya Dollars za Kimarekani Milioni 41.1
ambao ni Mkopo wa gharama nafuu kutoka Serikali ya India.
Naibu
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akisaidia uchimbaji moja ya
Mfereji utakaotumika kutandika mabomba katika eneo la mradi wa Maji,
Chalinze.
Naibu
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiwa pamoja na Afisa Mtendaji
Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA),
Mhandisi Cyprian Luhemeja na Msimamizi wa Mradi wa Maji, Chalinze,
Mhandisi Modesta Mushi katika eneo la mradi huo.
Naibu
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) (aliyevaa Kofia) akishuka chini
pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Bi. Zainabu Kawawa (aliyevaa Koti)
baada yakukagua moja ya Tenki lililopo kwenye Mradi wa Maji, Chalinze
mkoani Pwani.
Naibu
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiteta jambo na Afisa Mtendaji
Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA),
Mhandisi Cyprian Luhemeja.
Moja ya Tenki lililopo kwenye utekelezaji wa mradi wa Maji, Chalinze.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...