Shirika
la RAFIKI SDO ‘Rafiki Social Development Organization’ limekabidhi
vitendea kazi ikiwemo baiskeli 76 na mabegi 76 vyenye thamani ya
shilingi milioni 19.4 kwa wasichana na wanawake ‘Wawezeshaji wa vikundi’
kwenye wilaya ya Shinyanga ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao
vizuri katika mitaa na vijiji wanavyohudumia.
Hafla
fupi ya makabidhiano ya vitendea kazi hivyo imefanyika leo
Jumatano,Januari 23,2019 katika ofisi ya RAFIKI SDO mjini Shinyanga
ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko
kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack.
Awali
akizungumza, Mkurugenzi Mtendaji wa RAFIKI SDO, Gelard Ng’ong’a alisema
vitendea kazi hivyo vitatumika kwenye kata ambako shirika lao
linatekeleza shughuli za miradi ya maendeleo na kuongeza kuwa baiskeli
hizo zinakamilisha idadi ya baiskeli 148 kwani tayair walishatoa zingine
72.
“Wawezeshaji
hawa 76 tuliwapa elimu,sasa wanakwenda kuunda vikundi vya wasichana
wenye umri wa miaka 15 hadi 24 kwa ajili ya kuwafundisha masuala ya
ujasiriamali,malezi,mabadiliko ya tabia na masuala mtambuka,watatumia
vitendea kazi hivi kuwafikia wananchi kwenye maeneo yao kwenye
halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga”,alisema
Ng’ong’a.
“Shirika
letu limeajiri wawezeshaji wa vikundi 131 kwa kipindi cha kuanzia mwaka
2016 hadi 2019,kati ya 72 ni wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na
59 halmashauri ya Shinyanga,tunawapatia mishahara kila mwezi,wanalipiwa
NSSF na wameunganishwa na mfuko wa huduma za afya”,aliongeza Ng’ong’a.
Kwa
upande wake,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko alilipongeza
shirika la RAFIKI SDO kwa kushirikiana na serikali katika shughuli za
maendeleo huku akibainisha kuwa shirika hilo linatekeleza Ilani ya Chama
Cha Mapinduzi katika kuwezesha wananchi kiuchumi.
Mboneko
aliwataka Wawezeshaji hao kutumia vyema vitendea kazi walivyopatiwa
,kuomba mikopo kwenye halmashauri na kuhakikisha wanatumia mikopo hiyo
kwa shughuli za maendeleo.
Mkuu
huyo wa wilaya alitumia fursa hiyo pia kuwahimiza wanawake kutoa
taarifa za vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto huku
akiwashauri kutumia mikusanyiko ya watu kutangaza na kuuza bidhaa
wanazotengeneza.
Aidha
aliwaagiza maendeleo ya jamii kutembelea vikundi vilivyoanzishwa na
kuvishauri huku akizitaka halmashauri kushirikiana na mashirika yasiyo
ya kiserikali yaliyo mstari wa mbele kwenye masuala ya maendeleo.
Nao
wawezeshaji hao walilishukuru shirika hilo kuwa karibu nao na kueleza
kuwa hivi sasa wameweza kuanzisha biashara ndogo ndogo kwa ajili ya
kujiinua kiuchumi lakini pia tabia hatarishi zimepungua na wanaendelea
kupaza sauti juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akimkabidhi begi na baiskeli
Anna Kulwa kutoka kijiji cha Kizungu kata ya Lyamidati halmashauri ya
wilaya ya Shinyanga . Wa kwanza kushoto ni Afisa Maendeleo halmashauri
ya wilaya ya Shinyanga, Deus Mhoja na Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa
ya Shinyanga, Jackson Njau, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa
RAFIKI SDO, Gelard Ng’ong’a wakishuhudia zoezi la makabidhiano ya
vitendea kazi.
Anna Kulwa akishikana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa RAFIKI SDO, Gelard Ng’ong’a.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikabidhi vitendea kazi kwa
Rahim Ibrahim kutoka kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga.
Baiskeli na mabegi yaliyotolewa na RAFIKI SDO kwa wawezeshaji wa vikundi.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa hafla ya
makabidhiano ya vitendea kazi vilivyotolewa na shirika la RAFIKI SDO kwa
Wawezeshaji wa vikundi katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na
Manispaa ya Shinyanga. Kulia ni Afisa Tawala wilaya ya Shinyanga,
Charles Maugira.
Mkurugenzi
Mtendaji wa RAFIKI SDO, Gelard Ng’ong’a akizungumza wakati wa
makabidhiano ya vitendea kazi kwa wawezeshaji wa vikundi.
Kulia
ni Msaidizi wa Meneja shirika la RAFIKI SDO, Neema Lweeka akielezea
kuhusu shirika hilo na shughuli za maendeleo wanazotekeleza hususani
miradi ya afya,elimu,uwezeshaji kiuchumi,ulinzi wa mtoto,haki na utawala
na utoaji elimu ya stadi za maisha.
Wawezeshaji wa vikundi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiagana na wawezeshaji wa vikundi.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...