Mkuu Wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro amendelea na ziara yake ya kukagua ujenzi wa madarasa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza katika kata ya Bwawani.

Dc Muro akiwa katika ziara hiyo ameeleza kuwa wanafunzi zaidi ya 245 mpaka sasa wote waliopangwa kuingia kidato cha kwanza mwaka 2019 katika shule ya Sekondari Bwawani wamepata nafasi ya  kuendelea na masomo yao bila hata mmoja wao kukosa.

Ziara  ya Mkuu wa wilaya  Ndugu Jerry Muro imelenga kufahamu upatikanaji wa Elimu bora  kwa wanafunzi waliochaguliwa kidato cha kwanza kwa mwaka huu.

Pia Dc Muro amewapongeza wananchi wa kata ya bwawani kwa jitihada zao kuweza kujenga madarasa mawili kwa kipindi cha muda mfupi na kuanzia wiki ijayo wanafunzi wataanza kutumia madarasa hayo.

Sambamba na hapo Mkuu wa Wilaya hiyo ametoa wito kwa wananchi wote na wadau  mbalimbali wa maendeleo Wilayani Arumeru kuendelea kuchangia ujenzi wa madarasa pasipo kuvunjwa moyo na Baadhi ya wanasiasa wanaojaribu kuhujumu zoezi la ujenzi wa madarasa.
 Mkuu Wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro akitoa maelekezo kwa watendaji,wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa madarasa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza katika kata ya Bwawani.
 Mkuu Wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro akikagua ujenzi wa madarasa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza katika kata ya Bwawani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...