Na Ripota Wetu,Blog ya jamii
MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro,Rosemary Staki Semanyule, ametoa maagizo kwa wanavijiji kuhakikisha mashamba matano ambayo yamebainika kuwa na mirungi katika Kijiji cha Rikweni ndani ya Kata ya Tae ing'olewe.
Ametoa maqizo hayo baada yankubainika kuwa na kuna mashamba ya mirungi walipokuwa kwenye ziara ya kamati ya Usalama na wataalamu iliyofanyika katika kijiji cha Rikweni Kata ya Tae.
Akifafanua zaidi Mkuu wa Wilaya hiyo ya Same amesema lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kukagua uchimbaji barabara lakini wakao a kuna kuona mashamba ya mirungi na kuamua kuenda kung'oa mirungi kwa msaragambo ambayo wenye mashamba hayo wamekuwa sugu na kuyaacha bila kung'oa.
Hivyo ameagiza hadi Januari 11, 2019 mashamba matano yaliyobaki na mirungi yawe yameng'olewa ambapo pia amewataka viongozi wa vijiji kusimamia na kuwa wakishindwa kung'oa, basi wananchi watang'oa badala yao.
" Ili kujenga uzalendo wa kila mmoja kusimamia sheria. Kwani nao hawatoi taarifa kuhusu wahalifu.Tumepunguza mirungi toka vijiji 46 hadi 8 sasa. Navyo ni watu wachache, na tutahakikisha tunaimaliza kaabisa," amesema.
Ametoa mwito kuwa vijiji/vitongoji vya Tae, Belle, Mmeni, Irete, Kisesa, Makasa na Vudee kuondoa mirungi michache iliyobaki na kwamba hakuna watakaemuacha salama.
" Same isiyo na mirungi, inawezekana"
Baadhi ya wanavijiji wakihakikisha mashamba matano ambayo yamebainika kuwa na mirungi katika Kijiji cha Rikweni ndani ya Kata ya Tae inang'olewe.
Baadhi ya wanakijiji wakijadiliana jambo .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...