Na Vero Ignatus Arusha
Kanisa
la Tanzania Assemblies of God (TAG) limetoa mifuko 500 ya saruji ili
kusaidia ujenzi wa madarasa katika shule za sekondari zenye uhaba wa
madarasa licha ya kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi waliofaulu kujiunga
na kidato cha kwanza mkoani Arusha.
Askofu
Mkuu wa Kanisa hilo Dr.Barnabas Mtokambali amekabidhi mifuko hiyo kwa
mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ikiwa ni kuunga mkono jitihada za
serikali katika kuziba pengo la upungufu wa madarasa,ambapo amesema kuwa
kanisa hilo limeaona lishiriki katika maendeleo ya jamii kwa kusaidia
ujenzi wa madarasa.
Alisema
kuwa kanisa linatambua juhudi zinazofanywa na serikali katika kutoa
elimu kwa Watanzania hivyo wameamua kuungana na serikali kwa kutoa
mifuko hiyo kama chachu ya maendeleo ya elimu katika mkoa wa Arusha.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema kuwa kanisa la TAG limekua la
kwanza katika kutoa msaada kwa serikali na kuwezesha ujenzi wa madarasa
kwani ufaulu umeongezeka kwa kiasi kikubwa huku madarasa yakiwa
machache.
Gambo
alisema kuwa serikali inatambua mchango wa taasisi za dini katika
maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla hivyo wataendelea kushirikiana
katika kuwahudumia Watanzania.
“Taasisi
za dini ni wadau wakubwa wa maendeleo ambao licha ya miradi ya
kuhudumia wananchi bado wanaliombea taifa amani ambayo ni nguzo muhimu
kwa maendeleo ya taifa” Alisema Gambo
Muumini
wa Kanisahilo Danford Massawe alisema kuwa makanisa yanapaswa kuiga
mfano wa kanisa la TAG katika kushirikiana na serikali katika masuala ya
maendeleo ili kuharakisha maendeleo.
1.Picha Wakwanza kushoto ni mkuu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God nchini Tanzania Dkt. Barnabas Mtokambaki akimkabithi mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo mifuko 500 ya Saruji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...