Mkurugenzi wa  Biashara ya  DCB, Zacharia Kapama (wa pili kushoto)
 akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati akitangaza benki hiyo kupata faida ya kabla ya kodi ya Sh. Bilioni 1.9 kwa  mwaka 2018.Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano, Rahma Ngassa, Mkurugenzi wa Biashara, James Ngaluko na 

Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Ndani, Deogratius Thadei.
Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya DCB, James Ngaluko (wa pili kulia), akizungumza katika hafla hiyo. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Rahma Ngassa, Mkurugenzi wa Fedha, Zacharia Kapama na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Ndani, Deogratius Thadei.

Na Bakari Madjeshi,Globu ya jamii
BENKI ya Biashara ya DCB imesema imefanya juhudi za maksudi kuhakikisha inatoka kwenye hasara waliyoipata mwaka 2017 ambapo sasa imetangaza kupata faida ghafi ya Sh.bilioni 1.9  katika mwaka wa fedha 2018.

Faida hiyo ni baada ya mapato halisi ya riba kuimarika na uboreshaji wa huduma za mfumo wa kidigitali ambazo zimeongeza idadi ya wateja nchini nzima.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Fedha wa benki hiyo,Zacharia Kapama amesema faida hiyo ambayo wameipata imeipiku hasara iliyopatikana mwaka 2017 ya Sh.bilioni 6.9.

"Benki imefanya juhudi za makusudi kuhakikisha inatoka kwenye hasara iliyopatikana mwaka 2017 na kurudi kwenye faida baada ya kuchukua hatua kadhaa ikiwemo ya kuongeza kasi ya ukusanyaji madeni, "amefafanua Kapama.

Ameongeza mapato ya riba yaliimarika kutokana na utoaji wa mikopo katika sekta mbalimbali na kuchangia ongezeko la mikopo ghafi kutoka Sh.bilioni 88.6 mwaka 2017 hadi Sh.billion 90.6 mwaka 2018.

" Mikopo ya jumla ya Sh.billioni 65 imetolewa mwaka 2018 na kati ya fedha hizo Sh.billion 21 ilitolewa kwa wajasiriamali wadogo.Tumeongeza uboreshaji wa mfumo ya uendeshaji biashara kupitia mfumo wa kijidigitali na mkazo ukiwekwa katika kuogeza amana za gharama nafuu kupitia bidhaa za amana za kijiditali na usimamizi wa mizania wenye ufanisi,"amesema.

Ameongeza kwamba gharama za amana zimeshuka kutoka Sh.bilioni 9.8 billioni mwaka 2017 hado kufikia Sh.bilioni 6.8 mwaka jana. Pamoja na mambo mengine pia benki hiyo imeongeza ufanisi katika huduma na bidhaa zake zitolewazo kwa jamii.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Biashara wa Benki hiyo, James Ngaluko amesema waliongeza kasi katika utendaji na kuchangia upunguaji wa gharama za uendeshaji kutoka Sh.bilioni 21.2 mwaka 2017  kufikia Sh.bilioni 16.9  mwaka jana.

"Huduma za kidigitali zimekuwa chachu ya kuongeza ufanisi na kupunguza gharama za uendeshaji na gharama za riba, hizi ni kama vile akaunti kidijiti, DCB kibubu digitali na DCB FDR digitali akaunti,
akaunti hizi zinamuwezesha mteja kufungua akaunti na kufanya miamala yote ya kibenki, kutunza pesa na kuwekeza kwa kutumia simu yake ya mkononi," ameongeza Ngaluko.

Amesisitiza benki imeendelea kukua kwa kasi na kuongeza idadi ya matawi yake kufikia nane likiwepo tawi la Dodoma na wateja kuongezeka kutoka 144,475 mwaka 2017 kufikia 175,2014 mwaka jana na kuchangia ongezeko kubwa la miamala.

"Tumeweka malengo ambayo yatatufikisha kule ambako tunataka kwenda .Pia nieleze tu benki yetu imeendelea kukua kwa kasi ikiwa pamoja na kuengeza matawi hadi kufikia nane.Miongoni mwa matawi hayo limo tawi la Dodoma," amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...