Na Agness Francis, Blogu ya jamii.
UONGOZI wa shirika lisilo la Kiserikali la FEMINA umefanya sherehe za kutimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1999. Shirika hilo ambalo limeweza kufikia malengo yao ya kuwafikia vijana wengi zaidi katika kila Wilaya iliyopo Tanzania bara na baadhi ya shule za Visiwani Zanzibar na kutoa elimu ambayo imewasaidia na wengi wao kutoa mirejesho chanya kwa shirika hilo.
Hata hivyo shirika hilo limejikita katika utoaji wa elimu kwa vijana kuhusiana na afya ya uzazi na ujinsia kwa kuwapa stadi za maisha na kuwafundisha mbinu ya kusubiri hadi watakapotimiza malengo yao bila kujihusisha na masuala la ngono zembe.
Akizungumza katika hafla hiyo katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam Waziri wa Afya, Maendeleo, Jamii, Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalim amesema kuwa Serikali imekuwa mstari wa mbele kuunga mkono asasi za Kibinafsi kwa kutekeleza mipango, sera ya maendeleo ya watoto katika kuleta elimu kwa vijana ambao ni Taifa la kesho.
Aidha Waziri huyo amepongeza uongozi wa taasisi ya FEMINA kwa kuweza kufikia klabu zaidi 2300 hapa nchini ambazo zimesajiliwa na zimekuwa zikipata majarida pamoja na mafunzo mbali mbali yanayomuelimisha Kijana wa leo.
"Wazazi wengi siku hizi wamejisahau katika kutoa elimu ya jinsia kwa watoto wao, lakini nawapongeza Femina kwa kuweza kubeba majukumu ya wazazi hao kwa kutoa elimu, mbali mbali hasa katika ukuaji wa mtoto anapolekea kubalehe"amesema Ummy Mwalim.
Nae Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi ,Vijana, Ajira na wenyeulemavu, Stella Ikupa hakuwa nyuma katika kutoa pongezi kwa uongozi wa shirika la Femina Kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuelemisha jamii, na kuwataka wazidi kuongeza nguvu zaidi ili kuokoa Vijana.
"Kwa kazi nzuri inayofanywa na taasisi hii nawaomba waweze pia kujikita katika maeneo ya kupinga vikali madawa ya kulevya na athari zake, uwezeshwaji, kuhamasisha kujiajiri, kwenye upande wa Kilimo pindi Vijana hao wanapotoka masomoni"amesema Naibu Stella Ikupa.

Waziri wa Afya, Maendeleo, Jamii, Jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalim akiwapongeza viongozi wa Femina Hip kwa kutimiza miaka 20 ya taasisi hiyo na kazi nzuri wanayofanya kuelimisha jamii kwa ujumla, katika hafla ya sherehe iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Habari wa FEMINA Amabilis Batamula akizungumzia miaka 20 ya shirika hilo ilivyokuwa ya mafanikio makubwa kwani tangu kuanzishwa kwake mwaka 1999 kuwa vijana wengi wamenufaika na wanaendelea kulea Vijana wapya, mwishoni mwa wiki Jijini Dar Es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...