Mkuu wa Jeshi la Magereza Tanzania, Kamishna Jenerali Phaustine Kasike amesema wanaendelea na mpango wa kuhamisha wafungwa kutoka kwenye magereza yasiyo na shughuli za kilimo na kuwahamishia kwenye Magereza ya kilimo ili kufikia malengo ya kimkakati ya kuzalisha chakula kwa ajili ya kutosheleza wafungwa na mahabusu wote hapa nchini.
Ameyasema hayo mara baada ya kukagua shamba la mahindi la Gereza la Kitai lililopo katika Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma ambapo gereza hilo pia ni miongoni mwa magereza 10 hapa nchini, ambayo yameteuliwa kwenye mpango mkakati wa mradi wa kilimo kwa ajili ya chakula cha wafungwa na mahabusu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...