Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemank Jafo amesisitiza Viongozi na watendaji kutembelea miradi ya maendeleo inayo tekelezwa katika maeneo hayo ili miradi hiyo iweze kutekelezwa vizuri Kama inavyotakiwa.
Waziri Jafo aliyasema hayo Leo hii alipokuwa katika ukaguzi wa miradi ya DMDP wilayani Temeke Jijini Dar es Salaam.
Ziara hiyo ya kikazi ya waziri wa TAMISEMI ni muendelezo wa kazi tokea kuanza kwa mwaka 2019 iliyoanzia Wilayani Chemba, Kilosa, Kibiti, Rufiji, na Temeke.
Katika ziara hiyo Jafo alifanikiwa kufanya ukaguzi wa barabara za DMDP katika Kata ya Buza, ujenzi wa kituo cha afya Buza, pamoja na soko la kisasa linalojengwa eneo la Makangarawe.
Katika ukaguzi huo Jafo alifurahishwa Sana na kazi nzuri inayo tekelezwa katika eneo hilo. Ameagiza kituo hicho pamoja na soko hilo la kisasa likamilike kabla mwezi June mwaka 2019.
Waziri Jafo anaendelea na ziara ya kikazi mkoani Kigoma kwa lengo la kufuatilia thamani ya fedha zilizotewa chini ya ofisi ya Rais TAMISEMI kutekeleza miradi ya maendeleo katika Halmashauri zote Nchini.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo(katikati) akikagua
barabara zinazokengwa na mradi wa Dmdp katika kata ya Buza eneo la
Makangarawe
Soko la kisasa linaloendelea kujengwa katika Kata ya Buza eneo la Makangarawe kupitia mradi wa Dmdp
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo(katikati) akikagua
ujenzi aa Kituo cha Afya kinachojengwa katika Kata ya Buza

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...