Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani Jokate Mwegelo ameanza ugawaji wa vitambulisho vya wajasiriamali wadogo wilayani humo kwa lengo la kuhakikisha wanatambuliwa na kufanya shughuli zao za kiuchumi bila kusumbuliwa.

Jokate ametoa vitambulisho hivyo leo kwa baadhi ya wajasiriamali wa Wilaya ya Kisarawe ikiwa ni siku chache tu zimepita tangu Rais Dk.John Magufuli alipozindua utoaji wa vitambulisho hivyo kwa kuwapa wakuu wa mikoa yote nchini ili vigawiwe kwa wajasiriamali.

Akizungumza leo wilayani hapo mbele ya wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Wilaya ambao wameshiriki kushuhudia tukio la ugawaji wa vitambulisho hivyo, Jokate amesema katika wilaya hiyo kuna wajasiriamali 502 na hivyo ugawaji huo utaendelea kwa kuhakikisha wote wanaostahili kuvipata wanapewa.

Amesema wilaya ya Kisarawe inatambua mchango wa wajasiriamali hao na kwamba wamedhamiri wote wapewe vitambulisho hivyo ambavyo pamoja na mambo mengine kwa wale ambao watakuwa na vitambulisho hivyo watafanyakazi zao za ujasiriamali bila kusumbuliwa.

"Mkuu wa Mkoa wetu wa Pwani ametukabidhi hivi vitambulisho kwa ajili ya kuwapatia wajasiriamali, hivyo leo tumeanza kuvigawa.Ni mchakato endelevu ambao tutaufanya kwa wakati na hapa kwetu tunao wajasiriamali 502, na wote tutawapa," amesisitiza Jokate.

Wakati huo huo amezungumzia mikakati ya Wilaya ya Kisarawe katika kuhakikisha wanapiga hatua ya kimaendeleo ikiwa pamoja na kuitangaza Wilaya hiyo ambayo ina fursa za kila aina za kiuwekezaji .

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwegelo akimkabidhi kitambulisho cha ujasiriamali mjasiriamali Indiana Mohamed Mnyukwa katika kikao cha RCC kinachofanyika mjini Kisarawe leo wilaya ya Kisarawe imeanza kutekeleza agizo la Rais Dk. John Pombe Magufuli aliyetoa vitambulisho kwa ajili ya wajasiriamali nchini kote.

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwegelo akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajasiriamali waliokabidhiwa vitambulisho vyao leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...