Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo amewapongeza
Viongozi, watendaji, na wananchi wa wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma kwa
utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo. Waziri Jafo amefurahishwa
Sana na ujenzi wa vituo vya afya vya Kagezi Mabamba kwani ujenzi wake
umekuwa mzuri Sana unaoendana na thamani ya fedha iliyo tolewa na
serikali.
Katika ziara hiyo waziri Jafo alimpongeza Sana mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Eng. Nditiye kwani amekuwa akiwahangaikia Sana wananchi wake katika upatikanaji wa miradi hiyo ya maendeleo.
Aidha, Waziri Jafo alimalizia ziara yake kwa kukagua miradi ya barabara ya Kibondo mjini pamoja na kutembelea shule ya sekondari Malagarasi ambapo ukarabati na ujezi wa miundombinu umefanyika shuleni hapo kwa gharama ya shilingi milioni 400.

Waziri Jafo akikagua barabara za changarawe zilizojengwa na TARURA Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Malagarasi wakimskiliza Waziri Jafo(hayupo pichani) alipowatembelea shuleni hapo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo(katikati) akisomewa taarifa wakati alipotembelea Kituo cha Afya Kibamba kilichopo Kibondo Mkoani Kigoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...