Bw. Stephen Mbundi, Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiongoza Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa majadiliano kwa ngazi ya Watalaam wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwa maandalizi ya Mkutano Maalum wa 38 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) utakaofanyika tarehe 30 Januari 2019 jijini Arusha. 

Mkutano huu utafuatiwa na ule wa Makatibu Wakuu tarehe 29 Januari 2019. Pamoja na mambo mengine mkutano wa 38 wa Baraza la Mawaziri utapitia na kujadili agenda mbalimbali ikiwa ni pamoja na taarifa ya utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa na Baraza hilo kwenye vikao vilivyopita; taarifa kutoka Ofisi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo; taarifa kuhusu masuala ya miundombinu, forodha na biashara na masuala ya utawala na fedha. 

Mkutano wa 38 wa Baraza la Mawaziri ni maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika jijini Arusha tarehe 1 Februari 2019. Kulia ni Bw. Eliabi Chodota, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Kijamii na kushoto ni Bw. Bernard Haule, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Wataalam (wa pili kushoto) akizungumza wakati wa mkutano wa maandalizi ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika kwenye Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha tarehe 28 Januari 2019 
Wajumbe kutoka Burundi wakifuatilia mkutano huo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwuliofanyika jijini Arusha tarehe 28 Januari 2019 ngazi ya wataalam
Wajumbe kutoka Kenya nao wakifuatilia mkutano wa wataalam 
Wajumbe kutoka Uganda wakiwa kwenye mkutano 
Wajumbe kutoka Tanzania nao wakifuatilia mkutano huo 
Wajumbe wengine kutoka Tanzania nao wakifuatilia mkutano 
Wajumbe wa Tanzania kutoka Wizara, Taasisi na Sekta mbalimbali wakishiriki mkutano kwa ngazi ya wataalam 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...