SHINDANO la
Benki ya NMB kuhimiza matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass'
linalojulikana kama 'MastaBata', limefanyika tena ikiwa ni droo ya tatu
ambapo wateja wa benki hiyo wameendelea kujishindia fedha taslimu kwenye
akaunti zao. Droo iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam imewapata
washindi wengine 20 waliojishindia kiasi cha shilingi 100,000/- kila
mmoja.
Akizungumza katika droo hiyo , Mtaalamu kutoka kitengo cha kadi cha Benki ya NMB, Florence Mchau alisema wateja wengine 20 wamejishindia shilingi 100,000/- kila mmoja katika droo hiyo ya tatu kuchezeshwa, baada ya kufanya malipo mbalimbali kwa kutumia mfumo wa 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass'.
Alisema wateja hao wamepatikana baada ya kuchezeshwa droo iliyojumuisha wateja wote wa NMB waliolipa au kufanya manunuzi kwa kutumia mfumo wa 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' na wao kujishindia kitita hicho.Aidha droo ya tatu iliyofanyika leo inakamilisha jumla ya idadi ya wateja 60 ambao hadi sasa wamejishindia shilingi 100,000/- kila mmoja, huku ikiendeshwa kwa wazi ambapo wateja wakipigiwa simu na kujulishwa kabla ya kuingiziwa fedha walizojishindia.
Hata hivyo, aliwataka wateja wa NMB kuendelea kutumia huduma hiyo, kwani kampeni hiyo inayotarajia kuwazawadia zaidi ya shilingi milioni 100 wateja wa NMB inaendelea na takribani wateja 200 watanufaika. Licha ya fedha zawadi nyingine ambazo washindi watajipatia ni pamoja na simu janja za kisasa 'Samsung S9+' na mwisho washindi wengine 3 kati yao wawili kujishindia safari ya mapumziko kwenda Dubai iliyolipiwa kila kitu na NMB.

Mtaalamu kutoka kitengo cha kadi cha Benki ya NMB, Florence Mchau (kushoto) akizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa Droo ya Tatu ya kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata'. Kulia ni Ofisa Mwandamizi Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo akisimamia droo hiyo. Katikati ni Saumu Rajabu kutoka Selcom.
Mtaalamu kutoka kitengo cha kadi cha Benki ya NMB, Florence Mchau (kushoto) akimjulisha kwa njia ya simu mmoja wa washindi wa Droo ya tatu ameshinda katika droo hiyo ya kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata'. Kulia ni Ofisa Mwandamizi Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo akisimamia droo hiyo. Katikati ni Saumu Rajabu kutoka Selcom.
Droo hiyo ikiendelea kuchezeshwa kushoto huku wakishuhudia
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...