Na Ahmed Mahmoud,Arusha.

Wadau nchini wametakiwa kutumia fursa ya mikutano ya kimataifa kuchochea utalii na biashara ili kukuza pato la taifa na kuleta maendeleo yanayotokana na fursa za mikutano,biashara na utalii.

Hayo yameelezwa jijini Arusha katika mkutano wa Wadau wa Utalii,Wafanyabiashara pamoja na wamiliki wa kumbi za mikutano uliongazia fursa zinazotokana na mikutano ya kimataifa katika kukuza biashara na utalii .

Mwakilishi wa taasisi ya sekta binafsi Tanzania (TPSF) Antony Chamanga alisema kuwa kwa sasa wanashirikiana na serikali katika kuhakikisha kuwa mikutano ya kimataifa inaleta tija nchini kwa Wafanyabiashara,wamiliki wa hoteli pamoja na kusababisha ongezeko la utalii.

Aidha alisema kuwa kwa sasa sekta binafsi inashiriki vyema katika maendeleo na kukuza vipato vya watu waliojiajiri katika biashara na utalii hivyo mpango wa kushirikiana na serikali utasaidia kukuza mapato ya taifa.

Mratibu wa mikutano ya kimataifa kutoka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dorothea Massawe licha ya soko la watalii kwenda mbugani kujionea wanayamapori bado tunahitaji kuwa na zao lingine la mikutano ya kimataifa .

“Tukipata mkutano wa watu 1000,2000 kati yao wako watakaokwenda kutembelea vivutio vya utalii kama lilivyoagizo la serikali la kuongeza watalii bodi ya utalii inashirikiana na sekta binafsi katika kufanikisha biashara ya mikutano ya kimataifa” Alisema Dorothea

Mdau wa Hoteli Farida Hatibu anasema kuwa mkoa wa Arusha umekua kivutio kikubwa cha mikutano na watalii ambao hupendelea huduma zilizoko hivyo ubora wa huduma za mikutano ya kimataifa na miundombinu utasaidia kuvutia mikutano ya kimataifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...