Mkazi Bariadi Mkoa wa Simiyu, Golesu Maduhu (23) ameshinda Sh 56,137,550 baada ya kubahatisha kwa usahihi mchezo wa Perfect 12 unaoendeshwa na Kampuni ya M-Bet Tanzania.

Maduhu ameweza kubahatisha matokeo ya droo ya Desemba mwaka jana na kuwa mshindi wa kwanza kuzawadiwa fedha kutoka kampuni ya M-Bet kwa mwaka huu. Maduhu alipatia kiusahihi michezo yote 17.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fedha zake, Maduhu alisema kuwa amefurahi sana kupata kiasi hicho cha fedha ambacho kitamsaidia katika maisha yake. Maduhu amesema kuwa ametumia sh 1,000 kupata mamilioni hayo ya fedha na kuwaomba Watanzania kujiunga na michezo ya kampuni ya M-BET ambayo inachangia kubadili maisha. Meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi alisema kuwa katika fedha hizo, Serikali imepata Sh milioni 11.2 ikiwa ni kodi ya ushindi. “Nawaomba Watanzania washiriki katika michezo ya kubahatisha ya M-bet ambayo mwaka 2018 iliwazawadia jumla ya washindi 20 ambao walipata mamilioni ya fedha na kubadili maisha yao,” alisema Mushi.

Mkuu wa Kitengo cha Kodi za Kubahatisha Mamlaka ya Mapato (TRA) mkoa wa Ilala, Shabani Rashid Mwanga naye aliwaomba Watanzania kushiriki katika michezo hiyo ili kuchangia maendeleo ya nchi. Mwanga alisema kuwa unaoposhinda kiasi chochote, serikali inapata kodi yake moja kwa moja na kuongezea fedha za kufanyia maendeleo nchini. “Naishukuru M-Bet ambayo kila mara imekuwa ikitoa washindi wamekuwa wakipata mamilioni ya fedha na kuchangia pato la Taifa, ni chanzo kizuri sana cha mapato kwa ajili ya maendeleo ya nchini,” alisema Mwanga.

Meneja wa Leseni na Huduma za Sheria wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini, Catherine Lamwai aliipongeza kampuni ya M-bet kwa kuweka kuendelea kupata washindi wengi na kujizolea mamilioni ya fedha. “Bodi ya Michezo ya Kubahatisha imekuwa ikifuatilia na kusimamia michezo ya kubahatisha kutokana na kupata washindi wengi. Wametufurahisha sana kutokana kuchangia pato la Taifa kupitia mchezo wa Perfect 12,” alisema Lamwai.

Mshindi wa Droo ya 20 ya mchezo wa Perfect 12 wa kampuni ya M-bet, Golesu Maduhu (wa pili kushoto) akipokea mfano wa hundi baada ya kushinda Sh milioni 56.1 kutoka kwa meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet, Allen Mushi (wa tatu kushoto) baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 17. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Kodi za Kubahatisha Mamlaka ya Mapato (TRA) mkoa wa Ilala, Shabani Rashid Mwanga na wa kwanza kulia ni Meneja wa Leseni na Huduma za Sheria wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini, Catherine Lamwai. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...