Anaandika Dixon Busagaga, Tarangire. 

MWANAMITINDO na muigizaji maarufu Marekani aliyewahi kung’ara katika taji la Miss Universe, Marisela De Montecristo aliwasili nchini hivi karibuni ametembelea Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na kupokelewa na Mkuu wa Idara ya Utalii katika Hifadhi hiyo.

Muda mfupi baada ya kuwasili Mwanamitindo huyo aliyekuwa ameongozana na Mama yake mazazi pamoja na anayetajwa kuwa mchumba wake ,alikabidhiwa zawadi mbalimbali yakiwemo mavazi maalumu yanayotumiwa na Jamii ya Maasai.

Marisela baada ya kutembelea mane mbalimbali ya Hifadhi hiyo wakiwemo wanyama alieleza furaha yake huku akiahidi kuwa balozi wa vivutio vya utalii atakavyotembelea hapa nchini .

Mrembo huyo ambaye kwa sasa anaishi Los Angels amesema lengo la kuja nchini kutembelea vivutio vya utalii ni pamoja na kuangalia fursa mpya ipatikanayo katika sekta ya Utalii Duniani pamoja na kuvitangaza.

Mwanamitindi huyo anaendelea na ziara yake hiyo ya kitalii katika Hifadhi ya Ngorongoro ambako atashuhudia maajabu ya wanyama katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Bonde la ufa la Ngorongoro (Ngongoro Creator).”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...