Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
ASASI ya Uzalendo nchini (AWAMATA) imemtunuku cheti cha uzalendo Rais Dkt. John Magufuli kwa kufanya vizuri katika kipengele cha uzalendo kwa mwaka 2018.
Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa City Garden jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Asasi hiyo Chief Daudi Mrindoko ameeleza kuwa Rais Magufuli amejitoa katika kupambana na rushwa pamoja na kuanzisha miradi mikubwa yenye lengo la kuboresha uchumi na hali ya wananchi wa kawaida, hivyo mchango wake unapaswa kutambuliwa, kuthaminiwa na kuheshimiwa.
Mrindoko amesema kuwa mipango ya Asasi hiyo ipo katika kueneza elimu ya uzalendo kwa kuanzisha chuo cha Uzalendo kitakachotoa Elimu ya Uzalendo, Ujasiriamali na kuwajengea vijana uwezo wa kujitegemea na kuwa zao bora kwa taifa.
Pia Asasi hiyo imetoa picha maalumu ya miradi iliyotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli katika kipindi cha mwaka 2018 na kuelezwa kuwa kuwa kasi anayoenda na Mh. Rais ni kuleta neema kwa wananchi wengi.
Mwenyekiti wa AWAMATA Chief Daudi Mwidadi Mrindoko (aliyeshika picha) na katibu wa taasisi hiyo Pilly Kimario(aliyeshika cheti kushoto) wakiwa kwenye picha ya Pamoja na wadau na washiriki wa mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam .
Mwenyekiti wa AMATA Chief Daudi Mwidadi Mrindoko (aliyeketi kushoto) na katibu wa Asasi hiyo Pilly Kimario(aliyeketi kulia)wakiwa Pamoja na wakurugenzi wapya wa Asasi waliotangazwa katika mkutano mkuu wa mwaka, jijini Dar es Salaam.
Cheti
cha pongezi na kutambua mchango kupitia kipengele cha uzalendo kwa
mwaka 2018 kilichotolewa na taasisi ya uzalendo nchini kwa Rais Dkt.John
Magufuli, jijini Dar es Salaam.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...