
Wanafunzi 53 kutoka katika Kituo cha Elimu ya Maendeleo ya Afya ( CEDHA) cha Jijini Arusha, walimu na Baadhi ya Wafanyakazi wa Tume ya Nguvu za Atomiki wakiwa katika picha ya Pamoja wakati wa hitimisho la mafunzo ya udhibiti na matumizi salama ya vyanzo vya mionzi
Na. Vero Ignatus, Arusha
Tume ya Nguvu za Atomiki nchini imeendesha mafunzo kwa wanafunzi 53 wa kituo cha elimu ya maendeleo ya Afya CEDHA juu ya matumizi ya mionzi
Mafunzo hayo yamefanyika makao makuu ya ofisi ya TAEC iliyopo Jijini Arusha kwa siku tatu yakiwa na lengo la kujifunza maswala mbalimbali yahusuyo faida, matumizi udhibiti na madhara yatokanayo na mionzi mahala pa kazi pamoja na sheria zake
Mafunzo yameendeshwa na TAEC kupitia wataalamu wake wafuatao
Bw Eng. John Ben Ngatunga - Mtafiti
Bw Simon Mdoe- Mtafiti
Bw Jerome Mwimanzi- Mtafiti
Bw Siwidhani Ndovi- Mtafiti
Kwa mujibu wa TAEC lengo kuu la mafunzo hayo ni kutoa elimu ya matumizi salama ya vyanzo vya mionzi ili kujifunza maswala mbalimbali yahusuyo faida, matumizi, udhibiti na sheria zake ili kuwawezesha wanafunzi hao kuelewa matumizi salama ya teknoljia ya Nyuklia na kujilinda pindi watakapokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kikazi hapo.
Peter Ngamilo ni Mkuu wa kitengo cha mawasiliano kutoka TAEC ameeleza Kutokana na ufuatiliaji wa Mara kwa mara ambao unaambatana na ukaguzi unaofanywa na TAEC ,mpaka hivi sasa hakuna athari zozote zilizojitokeza kwenye maeneo ya kazi isipokuwa tu kuna baadhi ya vituo vichache ambavyo vimekuwa vikikiuka utaratibu na tayari imeshavichukulia hatua za Kisheria.
Hatua mojawapo iliyochukuliwa na TAEC ni pamoja na kuvifungia ili visitoe huduma ambayo itapelekea kusababisha athari za madhara ya mionzi kwa Wafanyakazi na mazingira yanayozunguka
TAEC inapenda kuwakaribisha wananchi na wadau mbalimbali ili kupata elimu hiyo juu ya yanayohusu udhibiti usalama wa mionzi na matumizi sahihi ya teknolojia ya nyuklia hapa nchini


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...