NA MWAMVUA MWINYI, RUFIJI
TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU )mkoani Pwani, imebaini kuwepo kwa mtandao mkubwa unaosaidia kufanikisha utoroshwaji wa mazao ya misitu kwa njia ya rushwa. Naibu mkuu wa taasisi hiyo mkoani hapo, Sadik Nombo alizungumzia suala hilo baada ya kituo maalumu cha Ikwiriri, kupata taarifa ya kuwepo magogo ya mbao ya mti aina ya mninga yapatayo 20 yamefichwa kwenye nyumba moja katika Kitongoji cha Mtakuja ,kijiji cha Umwe Kaskazini yenye thamani ya sh. milioni 4,370,448 .
Alisema magogo hayo ,yamevunwa kinyume na taratibu na sheria ya misitu namba 14 ya mwaka 2002. . Kufuatia taarifa hiyo ,alisema kwamba, ofisi ya TAKUKURU imefanya uchunguzi wa haraka uliofanikisha kukamatwa kwa mfanyabiashara mmoja aliyekutwa na magogo hayo. Nombo alifafanua, kitendo hicho kunaisababishia serikali hasara hasa katika mapato yatokanayo na uvunaji na usafirishaji wa mazao ya misitu.
"Uchunguzi wa kubaini wahusika katika mtandao huo unaendelea ili wahusika wote waweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria" Alitoa wito wa kushirikiana bega kwa bega katika mapambano dhidi ya rushwa kwa kuendelea kutoa taarifa za vitendo vya rushwa kwani rasilimali za nchi zinalindwa.
Hata hivyo Nombo aliwaomba pia ,watumishi wa umma kuwa wazalendo na kuwa mstari wa mbele kulinda rasilimali za nchi na si kuwa wawezeshaji wa kusaidia utaifishaji wa mali ya umma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...