Na Said Mwishehe,Arusha

SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco), limesema kwa sasa huduma zake nyingi zinatolewa kidigitali kutokana na kukua kwa teknolojia na hivyo kwa kutumia mitambo iliyopo inawawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi.

Tanesco imesisitiza inatambua kazi ya kukua kwa teknolojia na hivyo nayo imeamua kujikita katika kuweka mitambo hiyo ya kisasa ili kwenda na kasi ya ukuaji wa teknolojia katika kuhudumia wananchi na kwa sasa utendaji kazi umekuwa wa ufanisi zaidi kutoka na uwepo wa mitambo ya kisasa.

Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji amewaambia wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini waliopo kwenye ziara ya kutembelea miradi ya umeme inayotekelezwa na Serikali katika Mkoa wa Arusha, amesema shirika hilo kwa sasa haliko nyuma katika kukua kwa teknolojia na hivyo mitambo mingi ambayo imefungwa kwenye vituo vya kusambaza umeme.

"Kama tulivyoona ni kwamba Tanesco tunakwenda sambamba na ukuaji wa teknonolojia, vituo vyetu vingi vimekuwa vya kidigitali .Kwa hapa Arusha vituo vyetu vingi mitambo ambayo imefungwa ni ya kisasa ukilinganisha na miaka ya huko nyuma.Watalaamu wetu wakiwa ofisini kupitia mitambo iliyopo kama kuna tatizo lolote kwenye njia ya umeme kompyuta itaonesha na hivyo inakuwa rahisi kushughulikia tatizo,"amesema Muhaji.

Amefafanua "Hivyo ikitokea gari imegonga nguzo ya umeme, mti umeegemea waya au vyovyote vile kupitia mitambo iliyopo itaonekana moja kwa moja, hii inasaidia kushughulikia matatizo mapema na hivyo kuondoa hata malalamiko kwani kabla mteja hajafika Tanesco kutoa taarifa , tayari watalaamu wetu wameshaona na kuchukua hatua."

Akizungumzia Mradi wa Kukarabati na Kuimarisha Mifumo ya Umeme Tanzania(TEDAP) Muhaji amesema kwa Mkoa wa Arusha kupitia mradi huo wamefanya maboresho makubwa kwa kutengeneza vituo vipya ambapo imesadia kuufanya mkoa huo kuwa na umeme wa ziada.

Ameongeza kwa sasa Arusha haina tatizo la umeme na ndio maana wanahamasisha watu kuwekeza kwa kujenga viwanda huku akiwahamasisha wananchi ambao wanahitaji kuunganishwa umeme kufika kwenye shirika hilo kutoa maombi yao.

Pia amesema Serikali kupitia Tanesco inatekeleza miradi mbalimbali ya umeme nchini ukiwamo mkoa wa Arusha na hivyo kuna kila sababu ya jamii kufahamu utekelezwaji wa miradi hiyo lakini zaidi amewahamasisha wanaotaka kuwekeza kupitia sekta ya viwanda hivi sasa nchi ina nishati ya umeme wa uhakika.

"Tumeamua kufanya ziara hii ya kuwaleta wahariri wa vyombo vya habari , kwanza waone kazi ambayo Serikali ya Awamu ya Tano inafanya katika kuboresha upatikanaji wa nishati ya umeme nchini, pili wawe wajumbe wa kutoa taarifa kwa Watanzania kuhusu kazi inayofanyika na hasa uwepo wa umeme wa ziada katika Mkoa huu wa Arusha.Miradi ya TEDAP inafanyika pia kwenye mikoa mingine kadhaa ukiwamo wa Dar es Salaam ambako nako kuna miradi ya umeme ambayo inatekelezwa na mingine imekamilika,"amesema Muhaji.

Mtaalam wa masuala ya umeme akifafanua jambo kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini(hawapo pichani) baada ya kutembelea kituo cha umeme cha Sakina kilichopo Ngatamtoni mkoani Arusha

Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO)Leila Muhaji(kushoto) akimsikiliza Meneja wa shirika hilo mkoa wa Arusha Mhandisi Herini Mhina(kulia) kuhusu huduma ya usambazaji umeme mkoani hapa wakati wa ziara ya wahariri wa vyombo vya habari walipotembelea moja kituo cha umeme ambacho kimejengwa kupitia mradi wa TEDAP.Katikati ni Meneja Mwandamizi Miradi Mhandisi Emmanuel Manibora.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...