Na Chalila Kibuda,Namanga Arusha.

MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) zimejidhatiti kulinda bidhaa za vyakula ,dawa, vipodozi pamoja na Kemikali katika kuhakikisha walaji wanapata huduma bora za bidhaa hizo.

Kulinda kwa bidhaa hizo ni pamoja na kuhakikisha Serikali haipotezi fedha kwa kuingiza bidhaa zisizo na ubora.

Hayo yamebainishwa katika kituo cha Namanga wakati wa Maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto pamoja na Taasisi zilizo chini ya wizara hiyo walipotembelea Kituo cha ukaguzi Namanga mkoani Arusha ikiwa ni Kampeni Tumeboresha Sekta ya Afya katika miaka mitatu ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika utekelezaji wa uwekezaji katika sekta hiyo.


Maafisa wa mpaka wa Namanga kati ya Tanzania na Kenya walieleza mikakati ya utoaji wa huduma za ukaguzi kutokana na serikali kuwekeza rasimali watu pamoja vitendea kazi katika kurahisisha utoaji wa huduma katika mpaka huo.

Meneja wa Mamlaka ya Chakula na dawa (TFDA) Benny John amesema ofisi ya Kanda imeendelea kutekeleza majukumu yake mbalimbali ikiwemo udhibiti wa bidhaa za Chakula, dawa vipodozi na vifaa Tiba kwa kuhakikisha wafanyabiashara wanafuata kanuni na sheria zilizowekwa katika masilahi mapana ya kulinda wananchi katika utumiaji wa bidhaa hizo. iki
"Udhibiti wa bidhaa zinazoingia nchini umeongezeka kwa wafanyabiashara kulipa Kodi na tozo za Serikali na Hivyo kuongeza pato la Taifa" alisema Kaimu Meneja huyo.

Nae Mkaguzi wa Dawa wa TFDA mpaka wa Namanga Elia Nyeura amesema takwimu za shehena katika kituo cha Namanga zimeongezeka kutoka shehena 724 hadi kufikia shehena 1223 kwa mwaka 2016/2018."Kwa nia ya Rais wa awamu ya tano ya kuwa Tanzania ya viwanda, bidhaa zinazodhibitiwa na TFDA na mamlaka zingine zilizosindikwa kwa kipindi cha miaka mitatu shehena zimeongezeka kutoka 429 hadi kufikia 640 kwa 2016 /2018 " amesema Nyeura na

Ameongeza kuwa, mamlaka imepunguza upotevu wa fedha za kigeni zinazotokana na bidhaa zisizofaa". Alisema.Hata hivyo amebainisha thamani ya bidhaa iliyokamatwa kuingizwa nchini kwa kutofuata utaratibu imepungua kutoka Milioni 630.3 hadi kufikia Milioni 24.7 kwa mwaka 2015/2018 .

Kwa upande wa Msimamizi wa Kituo cha Ukaguzi Namanga wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Michael Benarnd amesema kuwa kemikali bidhaa za kemikali zinazoingia na kutoka nchini lazima wazikague katika hicho pamoja na kuhakiki vibali vya usafirishaji wa bidhaa hizo.

Amesema kuwa mwaka 2016 walikagua mizigo ya Kemikali 1300 ikiwa 750 ya mizigo hiyo ilifuata utaratibu wa sheria sawa na asilimia 57 ya mizigo iliyofuta sheria , mwaka 2017 walikagua mizigo ya Kemikali 1450 ikiwa 1120 ya mizigo hiyo ilifuata utaratibu wa sheria sawa na asilimia 77.2 ya mizigo iliyofuta sheria na mwaka 2018 mizigo 1320 iliyofuata utaratibu 1237 sawa na asilimia 93.7.

Aidha amesema kuwa ofisi ya GCLA imekuwa na mikakati mbalimbali katika kuhakikisha kemikali zote zinafuata sheria ikiwa ni pamoja na kushirikisha wadau katika uapatikanaji wa taarifa.

Kaimu Meneja  TFDA Kanda ya Kaskazini, Benny John akionesha kielelezo cha ulinganifu wa bidhaa zilizoingia nchini (Istogram) kwa  Maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto pamoja na Taasisi zilizo chini ya wizara hiyo (hawapo pichani) walipotembelea Mpaka wa Namanga panapokaguliwa na  TFDA Kanda ya Kaskazini, Mkoani Arushai ikiwa ni Kampeni ya ‘ Tumeboresha Sekta ya Afya’ inayolenga kueleza mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli.
Kaimu Meneja  TFDA Kanda ya Kaskazini, Benny John akizungumza na  Maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto pamoja na Taasisi zilizo chini ya wizara hiyo (hawapo pichani) walipotembelea Makao makuu ya TFDA Kanda ya Kaskazini, Mkoani Arushai ikiwa ni Kampeni ya ‘ Tumeboresha Sekta ya Afya’ inayolenga kueleza mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli.
 Meneja wa Mawasiliano na Elimu kwa Umma wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Gaudensia Simwanza akizungumza katika kituo cha Namanga  wakati Maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo katika Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya kwa kuangalia uwekezaji uliofanywa na serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Dkt John Pombe Magufuli katika miaka mitatu.

Mkaguzi wa Dawa wa TFDA mpaka wa Namanga Elia Nyeura akielezea taarifa fupi kwa   Maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto pamoja na Taasisi zilizo chini ya wizara hiyo (hawapo pichani) walipotembelea Mpaka wa Namanga panapokaguliwa na  TFDA Kanda ya Kaskazini, Mkoani Arushai ikiwa ni Kampeni ya ‘ Tumeboresha Sekta ya Afya’ inayolenga kueleza mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli. Anayefuatia ni Kaimu Meneja TFDA Kanda ya Kaskazini, Benny John
 Afisa Ukaguzi katika Kituo cha Namanga wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali GCLA, Michael Benarnd  akizungumza namna wanavyodhibiti uingiaji wa kemikali nchini katika kituo hicho, wakati Maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo walipotembelea kituo cha Namanga.

mkaguzi wa dawa wa TFDA kituo cha Namanga akiendelea na majukumu yake katika tukio hilo
 Afisa Ukaguzi wa TFDA akionesha Maabara hamishika wanavyotumia katika ukaguzi wa dawa,vifaa tiba pamoja vitendanishi katika kituo cha Ukaguzi wa pamoja cha Namanga. 
 Maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Kanda ya Kaskazini ya TFDA iliyopo mkoani Arusha.
Picha ya pamoja ya maofisa habari wa wizara,taasisi pamoja na maofisa wa kituo cha Namanga wakiwa nje ya kituo hicho mara baada ya kuona kazi zinazofanya kwenye kituo hicho

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...