Timu
ya kitaifa ya kushughulikia migogoro ya wakulima na wafugaji imefanya
ziara wilayani Mkuranga ,lengo ikiwa ni kutatua migogoro ya aina zote
za ardhi na kuiainisha.
Akizungumza
wakati wa ziara wilayani Mkuranga mkoa wa pwani,kiongozi wa timu ya
serikali ya ufuatiliaji wa migogoro ya wafugaji na watumiaji wengine wa
ardhi Dkt.Martin Ruheta amesema timu hiyo sio ya kisiasa bali ni ya
kitendaji na matarajio yao mpaka ifikapo 2020 itakuwa imepatiwa suluhu
kama sio kwisha kabisa.
Aidha
Dkt.Ruheta amewaahidi wanachi hao kuwa watahakikisha migogoro yao
inapatiwa ufumbuzi wa kudumu kwa sababu tume yao ipo makini.
Kwa
upande wake katibu wa mbunge wa jimbo la Mkuranga Omary kisatu
amewaomba wanachi hao kuwa na imani na tume hiyo."wakulima na wafugaji
naomba muendelee kudumisha amani na utulivu iliyopo,tume hii ni ya
kitaifa ya kuhakikisha haki ya mkulima na mfugaji inapatikana ."alisema
Kisatu
Hata
hivyo tume hiyo inaundwa na watu mbalimbali akiwemo Ofisa kutoka ofisi
ya Rais,Wizara ya Ardhi,Wizara ya mambo ya ndani ya nchi,Ofisa wa ardhi
na wa maliasili,lengo kuu ni kuhakikisha migogoro ya ardhi inakwisha
nchini
Kiongozi
wa Timu ya Serikali ya ufuatiliaji na Utatuzi wa Migogoro na watumiaji
wengine wa Ardhi Dkt.Martin Ruheta akizungumza na wakulima pamoja na
wafugjia wa kata ya Bupu wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.(Picha na
Emmanuel Massaka,MMG)
Kiongozi
wa timu ya Serikali ya ufuatiliaji,Utatuzi wa Migogoro ya watumiaji
wa Ardhi, Dkt.Martin Ruhete(kushoto) akiteta jambo na Katibu wa Mbunge
wa jimbo la Mkuranga,Omary Kisatu.
Katibu
Mkuu wa Chama cha wafugaji Tanzania, Magembe Makoye akiwasihi
wafugaji wa kijiji cha Matanzi kata ya Beta wilaya ya Mkuranga mkoa wa
Pwani, kutulia na kusubiri taratibu za serikali.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...