Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi alipowatembelea ofisini kwao makao makuu ya TPSC jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.

Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), Dkt. Henry Mambo, akieleza majukumu ya TPSC kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa TPSC cha kuhimiza uwajibikaji kilichofanyika Makao Makuu ya chuo hicho jijini Dar es Salaam.Mkuu wa Chuo na Mtendaji

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akikagua daftari la mmoja wa wanachuo wa Chuo cha Utumishi alipowatembelea wanafunzi hao katika moja ya madarasa ya Kampasi ya Dar es Salaam. Dkt. Mwanjelwa ametumia fursa hiyo kuwaasa wanachuo hao kusoma kwa bidii ili wawe watumishi wa umma bora hapo baadae.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akijaribu kutumia mashine ya kupiga chapa (typewriter) inayotumiwa kutolea mafunzo kwa wanafunzi wa TPSC alipotembelea moja ya darasa katika Kampasi ya Dar es Salaam ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwahimiza wanachuo wa TPSC waliopo maktaba kutumia vema maktaba hiyo ya chuo kujisomea ili kuongeza uelewa wa masomo wanayosoma, alipoitembelea maktaba hiyo iliyopo Chuo cha Utumishi Utumishi wa Umma Kampasi ya Dar es Salaam.



Watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kila mmoja kwa nafasi yake wametakiwa kutoa mafunzo bora yenye kuzingatia weledi, yatakayowajengea uwezo wa kiutendaji watumishi wa umma wanaopata fursa ya kujiendeleza katika chuo hicho ili waweze kutoa huduma bora na kwa wakati kwa wananchi.

Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati akizungumza na watumishi wa TPSC makao makuu na Kampasi ya Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji, kufahamu majukumu ya TPSC na kujiridhisha na utendaji kazi wa chuo hicho.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewahimiza watumishi wa TPSC kuwa wabunifu kwa kuboresha mitaala itakayowaandaa vema watumishi wa umma, sekta binafsi na wananchi wanaohitimu katika chuo hicho ili waweze kuwa na mchango katika maendeleo ya taifa. Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameongeza kuwa, katika ulimwengu wa sasa jamii inabadilika, uchumi unabadilika na siasa zinabadilika pia, hivyo amewataka watumishi wa TPSC wabadilike ili utendaji wao uwe wenye kujali matokeo na wenye tija.

Aidha, Dkt. Mwanjelwa alipata fursa ya kutembelea madarasa ya Kampasi ya Dar es Salaam ili kujionea vitendea kazi na kuzungumza na wanachuo ambao walimueleza kuwa, wanaridhika na elimu inayotolewa hivyo watatumia elimu na ujuzi wanaoupata katika kulitumikia taifa.

Naye, Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), Dkt. Henry Mambo amesema, TPSC ilianzishwa ili kusaidia zoezi la kujenga uwezo wa watumishi wa umma uwe wenye kujali matokeo katika kutoa huduma bora kwa umma na kuongeza kuwa, kwa sasa chuo kina matawi sita yaliyopo Dar es Salaam, Mtwara, Singida Tabora,Tanga na Mbeya.

Dkt. Mambo amefafanua kuwa, madhumuni makubwa ya kuanzisha chuo ilikuwa ni kuziba pengo lililokuwepo la kukosekana kwa chuo rasmi kinachoshughulikia mafunzo ya watumishi wa umma ili waendane na mabadiliko yaliyoletwa na maboresho katika utumishi wa umma na kuongeza kuwa lengo lingine lilikuwa ni kusaidia, kukuza na kuboresha stadi za wafanyakazi, kubadili mtazamo juu ya utendaji wa watumishi wa umma katika suala zima la utoaji huduma bora kwa umma unaolenga kukuza uchumi na kuondoa umaskini kupitia mafunzo ya muda mfupi na mrefu.

Dkt. Mambo ameainisha kuwa, tangu chuo kianzishwe mwaka 2000 kimeweza kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa watumishi 61,221 katika nyanja ya uongozi, menejimenti na utawala .Aidha, Dkt. Mambo amesema kuwa, chuo kimeruhusiwa kutoa mafunzo ya muda mfupi na mrefu kwa sekta nyingine ikiwemo sekta binafsi iwapo wana mahitaji ya kupata mafunzo ya kuwawezesha kuboresha utendaji kazi wao wa kila siku.

Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania ni Wakala wa Serikali iliyoanzishwa mwaka 2000 chini ya Sheria ya Wakala wa Serikali ya mwaka 1997. Kuanzishwa kwa Chuo cha Utumishi kunafuatia muungano wa Chuo cha Watumishi wa Serikali, Dar es Salaam (Civil Service Training Centre) na kilichokuwa Chuo cha Uhazili Tabora (Tabora Secretarial College). Chuo cha Utumishi wa Umma kipo chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...