Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Shirika la Taifa la Madini (Stamico) limesema kuwa litaendelea kusimamia sekta ya madini katika kutoa utaalam kwa wachimbaji wadogo katika kuhakikisha wanakua ikiwa ni pamoja kuongeza Pato la Taifa.

Akizungumza katika katika mahojiano na Michuzi Blog katika Mkutano wa Madini uliofanyika jijini Dar es Salaam ,Kaimu Mkurugenzi wa Uchorongaji na Utafiti Alex Rutagwelela amesema kuwa Stamico iko wazi katika kuhudumia wachimbaji wa Madini wadogo masaa 24.

Amesema kuwa wana mtambo wa uchorongaji ambapo wachimbaji wadogo ni wakati mwafaka wa kutumia kwa gharama nafuu.

"Wachimbaji wa madini wadogo watumie shirika lao katika ushauri ili kuweza kuchimba kisasa na kuchimba kimazoea wa bila mafanikio" amesema Rutagwelela.

Rutagwelela amesema kuwa mkutano wa Madini ulikuwa na maelekezo ya viongozi wakuu wa nchi hivyo kazi yetu ni kutekeleza maagizo ili sekta ya madini iwe nguzo ya uchumi kutokana na rasilimali zilizopo ziendelezwe kwa maendeleo.

Aidha amesema kuwa Stamico imekuwa ikitembelea wachimbaji wadogo wa madini kuwataka kushirikiana katika kuwapa ushauri.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC)Dkt. Samuel Gwamaka amesema kuwa suala uchimbaji wa madini linakwenda na mazingira.

Amesema kuwa mazingira ndio yanamzunguka mwanadamu hivyo lazima yalindwe na kusimamiwa.
Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Uchorongaji wa Shirika la Taifa la Madini (Stamico) Alex Rutagwelela akizungumza na waandishi habari katika mkutano wa Madini uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Usimamizi wa Mazingira Dkt. Samuel Gwamaka akizungumza kuhusiana na Baraza hilo katika usimamiaji wa Mazingira katika Sekta ya madini katika mkutano wa Madini uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari wa Shirika la Taifa la Madini (Stamico) Said Mtuwa akitoa maelezo kwa wadau wa Madini walipotembelea sehemu ya maonesho ya mkutano wa Madini uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...