WAKATI
Tamasha la Pasaka likijiandaa kuwasha moto katika Jiji la Dar es
Salaam, Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion na muandaaji wa Tamasha
la Pasaka Alex Msama ametoa mwito kwa wasanii mbalimbali nchini
wakiwamo wa muziki wa Injili kuhakikisha wanafuata na kuheshimu Sheria
za Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA).
Msama amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumzia msimu mpya wa Tamasha la Pasaka ambalo linatarajia kuanza Aprili 21,2019.Amefafanua tamasha hilo litaanzia Katika Jiji la Dar es Salaam na kauli mbiu ya tamasha hilo inasema Umoja na upendo huduma amani ya nchi yetu.
Kuhusu wasanii kufuata Sheria za BASATA, Msama ametoa mwito kwa wasanii kuiheshimu Baraza hilo na kwamba wasanii ambao watashiriki ni wale ambao wamejisajili na kutambuliwa kisheria.
Kuhusu tamasha hilo amesema BASATA tayari wametoa maelekezo yenye lengo kuhakikisha tamasha hilo linafanikiwa. "Siku zote usipokuwa na msimamizi huwezi kufanya vizuri, Wasanii wengi wanakuwa na dharau, bila BASATA tamasha hili lingekuwa limekufa siku nyingi", amesema Msama
Katika hatua nyingine, Msama amesema kuwa wapo kwenye mazungumzo na wasanii kutoka mataifa ya nje, kuhakikisha nao wanapata mualiko ili washiriki tamasha hilo.
"Wasanii wote ambao watashiriki ni wale wanaoiheshimu BASATA, ni vema wasanii wakahakikisha wanafuata sheria katika kufanya kazi zao za sanaa", amesema Msama .Msama muda si mrefu wataanza kutaja majina ya wasanii ambao watashiri tamasha hilo na kueleza kwa mwaka huu tamasha hilo litafanyika pia katika Jiji la Dodoma.
Wakati huo huo Msama amesema katika kipindi cha tamasha la Pasaka watatumia pia nafasi hiyo kuendelea kumuombea Rais Dk.John Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Serikali ya Awamu ya Tano.

Mkurugenzi
wa kampuni ya Msama
Promotions na muandaaji wa Tamasha la Pasaka Alex Msama
akizungumza na waandishi wa habari leo alipokuwa akifafanua mambo
mbalimbali kuhusu maendeleo ya Tamasha la Pasaka jijini Dar es
salaam,ambalo linatarajiwa kuanza kurindima Aprili 21,2019.
Mkurugenzi
wa kampuni ya Msama
Promotion na muandaaji wa Tamasha la Pasaka Alex Msama
akitoa ufafanuzi zaidi kuhusiana na wasanii watakaoshiriki kwenye
tamasha hilo ambalo kwa kawaida hufanyika kila mwaka,mbele ya waandishi
wa habari leo, jijini Dar es salaam,kushoto ni Mratibu wa Tamasha
hilo Jimmy Charles.
Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi
wa kampuni ya Msama
Promotion na muandaaji wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama alipokuwa
akizungumza nao leo jijini Dar kuhusu maendeleo ya maandalizi ya
tamasha na ujumbe muhimu kwa wasanii/waimbaji watakaoshiriki
tamasha hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...