Na Ripota Wetu, BBC

IMEELEZWA Wabunge nchini Uingereza wanajitayarisha kupiga kura iwapo kuunga au kutounga mkono mpango wa Theresa May wa kujitoa katika Umoja wa Ulaya.

Kura hiyo inayotajwa kuwa ni Kura yenye umuhimu ambayo itafanyika baadaye leo Januari 15, 2019 wakati mjadala wa siku tano kuhusu Brexit ukikamilika na kwamba May amewataka wanasiasa kuunga mkono mpango wake au kuhatarisha "kuwavunja moyo raia wa Uingereza".

Kwa mujibu wa Shirika la Habari nchini Uingereza(BBC) ni kwamba wabunge wake mwenyewe wakitarajiwa kujiunga na wa vyama vya upinzani kupiga kura dhidi ya mpango huo.Hata hivyo inatarajiwa mpango huo hautofaulu.Pia wabunge watapata fursa ya kutoa mapendekezo ya marekebisho ambayo yanaweza kuunda upya mpango huo kabla ya kura kuanza 19:00 kwa saa ya GMT.

Inaelezwa kuwa Waziri Mkuu aliwahotubia wabunge wake Jumatatu jioni katika jitihada za mwisho kujaribu kupata uungwaji mkono kwa mpango wake unaojumuisha mpango wa kujitoa kwa misingi ya ambavyo Uingereza itajitoa kwenye Muungano wa Ulaya na tangazo la kisiasa kwa uhusiano wa siku zijazo.

Awali, katika Bunge la wawakilishi, alisema: "Hauko imara kabisa lakini wakati historia itakapoandikwa, watu watatazama uamuzi wa Bunge hili na watauliza, 'Je tuliwajibika kuhusu kura ya taifa hili kujitoa katika EU, tuliuchunga uchumi wetu, usalama na muungano au tuliwavunja moyo raia wa Uingereza?'"

Hata hivyo May alijaribu kuwashawishi wabunge kuhusu mpango wenye mbadala wenye mzozo wa kuepuka kurudishwa kwa ukaguzi wa mipakani kati ya Uingereza na Ireland. 
 
 

KUSOMA ZAIDI  BOFYA BBC Swahili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...