WAHAMIAJI haramu 81 wamekamatwa wakiuza pipi, karanga na
kahawa na kujifanya machinga. Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake, Kaimu Afisa
Uhamiaji mkoa wa Dar es Salaam, Mrakibu Novaita Mrosso alisema kati ya
watu hao 35 ni raia wa Burundi ambao walikuwa wanafanya biashara hiyo
kama machinga kwa kutembeza sehemu mbalimbali.
Wahamiaji hao, wamekamatwa mwishoni mwa wiki na Idara ya Uhamiaji
wakifanya biashara hiyo jijini Dar es Salaam. Operesheni kali imekuwa inafanyika jijini zima ili kuhakikisha
wahamiaji wote wanatiwa mbaroni ambapo wahamiaji hao baadhi
wamejifanya machinga kukwepa kukamatwa. Hatua hiyo, imekuja baada ya mwishoni mwa mwaka jana, Rais Dkt. Magufuli kutoa vitambulisho maalum kwa ajili ya kuwatambua
wafanyabiashara wadogo wadogo nchini ambapo kila Mkuu wa Mkoa
alikabidhiwa.
Vitambulisho hivyo jumla 25,000 na kila kitambulisho kitagharimu
shilingi 20,000 kwa machinga.
Uhamiaji imeingia kazini baada ya kugundua kuwa wapo baadhi ya
wahamiaji haramu wamekuwa wanafanya biashara kama wamachinga na kazi
hiyo ilifanyika Januari 17, mwaka huu hadi Januari 20 ambapo jumla ya
watu 81 walikamatwa.
Mrakbu Mrosso alisema wahamiaji hao wamekuwa wanauza kahawa, karanga,
pipi na vitu vidogo sehemu mbalimbali za jiji huku wakijifanya kama
sehemu ya machinga kujificha.
"Tumewanasa na wanafikishwa mahakamani haraka kisha watarudishwa kwao,"alisema.
Aliongeza kuwa bado wanaendelea kuwahoji wahamiaji wengine 46 kujua
wanatoka nchi gani na kujua uhalali wao wa kuwepo hapa nchini.
"Hapa tumebaini wapo wasomali,wanigeria, Mcameroon na wengine,"alisema.
Mrakibu Mrosso alisema kazi ya kuwasaka wahamiaji haramu ni endelevu
na wamekuwa wanashirikiana na viongozi wa serikali za mitaa ili
kuwabaini wote.
"Nawaomba watu wenye taarifa watupe habari, sisi tutaendelea kuwaficha
wale wote wanaopa ushirikiano ili kuwakamata wahamiaji,kamwe hawaponi
tutawakamata wote na wale wanaowaleta,"alisema. Pia, amewaomba viongozi walioajiri wageni kutoa taarifa kwa vile hivi
sasa wanaendelea na kazi ya kupitia kila sehemu ikiwemo viwanda,ofisi,
baadhi ya makazi ili kuwanasa wageni wote wanaoishi kinyemela.
Alisema wamefanya kazi hiyo toka Novemba na Disemba,mwaka jana na
kuhakiki jumla ya wageni 16,102 ambapo 7,000 walihakikiwa katika ofisi
ya mkoa.Wengine 3,613 walihakikiwa katika ofisi ya Ilala, 3,668
Kinondoni,1,267 Temeke,356 Ubungo na 198 Kigamboni.
Mrakibu Mrosso alisema kwenye zoezi hilo,wamefanya utambuzi na
uandikishaji wa raia wa Malawi na wahamiaji walowezi ambapo jumla
waliandikishwa ni 1,770.
Kwenye mabao Kinondoni(756),Ilala (548)Temeke(162),Ubungo (144) na
Kigamboni ni 150.
Ametoa onyo kali kwa wananchi wanaohifadhi wahamiaji haramu kuacha
mara moja kwa vile mali zao na kifungo huenda kikawakumba. "Unajua sheria imebadilika hivi sasa kifungu cha 46 cha sheria
uhamiaji sura ya 54 rejeo la 2016,mtu akikamatwa amehifadhianaweza
kufungwa miaka 20,gari au nyumba inataifishwa pia na adhabu zote
zinaweza kuwa za pamoja,"alionya.
Wahamiaji haramu waliokamatwa mkoa wa Dar es Salaam wakiwa wamechuchumaa baada ya kufikishwa makao makuu ya uhamiaji.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
Kaimu Afisa Uhamiaji jijini Dar es Salaam, Novaita Edmund Mrosso akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wahamiaji haramu waliokamatwa maeneo mbalimbali ya jijini Dar es Salaam .
Kaimu kamishina wa Uhamiaji jijini Dar es Salaam,Novaita Edmund Mrosso akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...