Mkuu wa
mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amefafanua fursa mbalimbali za
uwekezaji zinazopatikana katika Mkoa hasa sekta ya kilimo kwa wahitimu
wa mafunzo kwa vitendo kutoka katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi
waliotembelea mkoani hapa ili kujionea maendeleo ya mkoa.
Wahitimu hao kutoka katika nchi kadhaa barani Afrika wamelenga kutembelea katika viwanda vikubwa vinavypoaptikana katika mkoa, maeneo ya uwekezaji wa kilimo, kufika kwenye vivutio vya utalii, machimbo ya makaa ya mawe pamoja na hifadhi za misitu.
Mh.Wangabo alisema kuwa uwekezaji wa kwenye viwanda unahitajika kwasababu ya uwepo wa mazao ya kulisha viwanda hivyo ikiwemo viwanda vya kuchakata mahindi, maharage na mpunga na kuwaondoa shaka juu ya upatikanaji wa umeme kwani hadi kufikia mwaka 2020 vijiji vyote vya mkoa wa Rukwa vitakuwa na umeme.
“Maeneo mazuri ya uwekezaji upo kwenye viwanda hasa viwanda vya kuchakata mazao ndani ya mkoa wetu, pia mwaka huu tuna zao la alizeti kama zao la Kimkakati ambapo hadi sasa kuna tani za mbegu zaidi ya 11,000 ambazo zimeshanunuliwa na wakulima na kupandwa na hivyo tunategemea uzalishaji mkubwa wa alizeti kwa mwaka huu na hivyo tunawaalika wawekezaji kuweka viwanda vya uchakataji wa alizeti ikiwa ni zao la kimkakati kwenye mkoa wetu.” Alisema.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Benard Makali (kulia) akipokea moja ya zawadi alizopewa na Uongozi wa chuo cha Ulinzi nchini ikiwasilishwa na Kiongozi wa Msafara huo Commodore M. Mumanga
Picha ya apmoja kati ya Wahitimu wa Chuo cha Ulinzi nchini pamoja na Wataalamu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa wakiongozwa na Mkuu wa mkoa Mh. Joachim Wangabo (wa tatu toka Kulia).
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia)akipokea moja ya zawadi alizopewa na uongozi wa chuo cha Ulinzi nchini kama shukrani ya kuwapokea vizuri katika Mkoa, zawadi iliyowasilishwa na Kiongozi wa Msafara huo Commodore M. Mumanga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...