Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Rosemary Staki Senyamule, amehimiza matumizi mazuri ya mafunzo ya Jeshi la Akiba kwa wahitimu wa mafunzo hayo kwa kuwataka kuwa mfano wa kuigwa ndani ya jamii.
Ametoa kauli hiyo wakati wa kufunga mafunzo ya Jeshi la Akiba wilayani Same ambapo pia amewasisitiza waliohitimu mafunzo hayo kuwa mfano wa kuigwa katika jamii na kufanyakazi kwa kujitolea.
Mkuu wa Wilaya huyo amewahakikishia waliohitimu mafunzo hayo kupewa kipaumbele usaili JKT na ajira wakiwa na sifa.
Pia amewaagiza kukomesha biashara ya mirungi na vibaka Makanya. "Hakikisheni kupitia mafunzo ambayo mmeyapata na kuzuia biashara ya mirungi."
Katika mafunzo hayo jumla ya wahitimu 108 wapata vitambulisho. Wananchi wametumia nafasi hiyo kupongeza utendaji kazi wa Rais Dk.John Magufuli kwani Makanya wana mradi wa maji unaendelea, waahidiwa fedha kuanza kidato cha tano.
Wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba wakila kiapo cha utii mbele ya Mkuu wa Wilaya Mh.Rosemary Staki Senyamule (hayupo pichani).
Picha ya pamoja
Mkuu wa Wilaya Mh.Rosemary Staki Senyamule Wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba wakiwa katika picha ya pamoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...