ZAIDI wa Wachama Wastaafu 5000 mkoani Tanga waliondikishwa kwenye Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuanzia Julai 2009 hadi Septemba 2018 wameanza kuhakikiwa.

Hayo yalisemwa leo na Meneja wa Mfuko mkoani Tanga Ally Mwakababu (Pichani Juu) wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema zoezi hilo lilianza Januari 2 mwaka huu na litamalizika Machi 30 mwaka huu.

Alisema kwamba uhakiki huo unafanyika kwa kipindi cha miezi mitatu huku akiwataka wastaafu mkoani hapa ambao walioandikishwa kufika kwenye ofisi za mfuko huo kwa ajili ya kuhakikiwa. Mwanachama Mstaafu afike ofisini akiambatana na mwenza wake (endapo yupo hai)endapo mwanachama mstaafu amefariki ,mwenza aliyebaki afike kwa ajili ya uhakiki huo “Alisema Meneja huyo.

“Lakini pia mwanachama anapaswa kufika na vitu muhimu ikiwemo kitambulisho cha NHIF, Cheti cha Ndoa (kwa mstaafu mwenye mwenza),Kitambulisho cha Uraia au mpiga kura ,leseni ya Gari au hati ya kusafiria ikiwemo barua ya kustaafu “Alisema Meneja huyo.

Hata hivyo alisema kwamba ofisi inawataka wanachama wastaafu kufika kwa uhakiki ndani ya muda uliowekwa ili kuepuka usumbufu wa kukosa huduma kwa kutokufanya hivyo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. mwanachama mstaafu wa NHIF anaestahili kupata matibabu yapasa awe na sifa zipi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...