*Wabunge waanza kuuchambua,Halima Mdee ataka Bunge kuchukua tahadhari
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi ,Vijana na Ajira
amewasilisha rasmi Bungeni Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya
Siasa ambapo baada ya kuwasilisha wabunge mbalimbali wameuchambua na
kutoa maoni yao.
Hata
hivyo baadhi ya wabunge hasa wa Vyama vya Upinzani ambao wamechangia
mjadala kuhusu muswada huo wametilia shaka baadhi ua vipengele na kuomba
Bunge kuviangalia kwa umakini mkubwa.
Wakati
anawasilisha Muswada huo wa Marekebisho ya Sheria vya Vyama vya Siasa
Waziri Mhaga ameliambia Bunge leo mjini Dodoma na lengo la muswada huo
ni kuwa na sheria ya vyama vya siasa ambayo itamuwezesha Msajili wa
Vyama vya Siasa kutekeleza majukumu yake vuzuri.
Amefafanua
baadhi ya vipengele vilivyopo kwenye muswada huo ambapo kabla ya hapo
aliweka wazi mchakato wa muswada huo ulianza rasmi mwaka 2013 na
ilipofika mwaka 2014 ulisimama kupisha mchakato wa Katiba Mpya na mwaka
2015 mchakato ukasimamishwa kupisha uchaguzi Mkuu.
"Muswada
wa marebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa wa mwaka 2018 unalenga
kufanya mabadiliko mbalimbali kwa lengo la kumuwezesha Msajili wa Vyama
vya siasa kufanya shughuli zake kwa ufanisi."
Kama nilivyotangulia kueleza awali mchakato ulianza mwaka 2013 wakati
ukusanyaji wa maoni na ilipofika mwaka 2014 ulisimama kwa ajili ya
mchakato wa Katiba mpya na mwaka 2015 ulisimama kupisha uchaguzi
mkuu.Muswada huu ninaouwasilisha leo hii umegawanyika sehemu kuu
mbili,"amesema Waziri Mhagama.
Amefafanua
muswada huo unampa nafasi Msajili wa Vyama vya Siasa kutekeleza
majukumu yake ambapo akatumia nafasi hiyo kuelezea hatua kwa hatua
vipengele vilivyomo kwenye muswada huo kikiwemo kipengele kinachovitaka
vyama vya siasa kuheshimu Katiba ya nchi pamoja na alama kuu za Taifa.
Pia
kuna vipengele ambavyo vinatoa maelekezo ya vyama vya siasa namna ya
kupata viongozi wake pamoja na hatua zinazotakiwa kufuatwa kwa anayetaka
kuanzisha chama cha siasa.
Katika
kipengele cha kuanzisha chama cha siasa moja ya sharti ni kwa
anayeanzisha kuwa raia wa kuzaliwa wa Tanzania ambacho kinakwenda
sambamba na uraia wa wazazi.Kipengele hicho kimeonekana kuibuq mjadala
Bungeni.
Pamoja na mambo
mengine muswada huo kwa mujibu wa Waziri Mhagama amesema unaweka
maelekezo ya jina la chama cha siasa kutofafana na chama kingine ili
kuepuka migongano kati ya chama na chama.
Pia
amesema muswada unaweka maelekezo ya jina la chama cha siasa kutofafana
na chama kingine.Pia muswada huo una kipengele ambacho kinataka vyama
vya siasa kuwasilisha orodha ya majina ya viongozi wa ngazi mbalimbali
pamoja na kuwepo orodha ya wanachama kwa lengo la kumuwezesha msajili
kuwa na kumbukumbu ya vyama husika.
Waziri
Mhagama pia amesema muswada huo una kipengele ambacho kinaeleza kuwa
ni marufuku kwa vyama vya siasa kuwa na vikundi vya ulinzi ambapo
kipengele hicho nacho kimeibua mjadala kwani wakati Mbunge wa Kawe
Halima Mdee(Chadema) wakati anachangia ameonesha kutoridhishwa na uwepo
wa kipengele hicho na kuomba Bunge na Kamati ya Katiba na Sheria
kuangalia upya kipengele hicho.
Wakati
huo huo Mdee wakati anacgangia muswada huo amesema si kweli kwamba
wabunge wa vyama vya upinzani pamoja na vyama vya siasa nchini
vinaukataa muswada huo kwani mwaka 2009 walipeleka muswada Bungeni
kutaka sheria ya vyama vya siasa kufanyiwa marekebisho.
"Kambi
ya upinzani bungeni mwaka 2009 tulipeleka muswada bungeni ili
kuhakikisha sheria ya vyama siasa inafanyiwa marekebisho lakini
ikakataliwa.Hatujawahi kuogopa kukaguliwa jana,leo na kesho,tuache
kutumia propaganda katika jambo la Nchi.
"Watu
hapa wanasema tusijadili mambo madogo,hivi kujadili jambo linalovunja
Katiba ni dogo?Ibara ya 8 C ya muswada huu kinavunja Katiba," amesema
Mdee na kufafanua kuna vipengele ambavyo vinaleta ubaguzi na hilo ni
huko ni kuvunja Katiba ya nchi.
Amezungumzia
pia kipengele ambacho kinataka kuwepo na orodha ya viongozi wa ngazi
mbalimbali kwa kupeleka orodha hiyo kwa Msajili sambamba na kuorodhesha
majina ya wanachama jambo ambalo ni gumu hasa kwa kuzingatia mwanachama
anaweza kujiunga leo na kesho akatoka kwenye chama husika.
Pia
ameonesha mashaka na kipengele cha kuzuia vyama vya siasa kuwa na
vikundi vya ulinzi ambapo anasema kipengele hicho hakubaliani nacho .



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...