Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya
Ujenzi ya CHICCO kutoka China inayojenga barabara ya Mbinga – Mbamba
bay kwa kiwango cha lami, yenye urefu wa Kilomita 66 wakati alipokagua
ujenzi wa barabara hiyo, Januari 4, 2019. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa
Ruvuma, Christina Mndeme.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
viongozi wa Mkoa wa Ruvuma na wafanyakazi wa Kampuni ya Ujenzi ya
CHICCO kutoka China inayojenga barabara ya Mbinga – Mbamba bay yenye
urefu wa Kilomita 66 wakati alipokagua ujenzi wa barabara hiyo, Januari
4, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipokagua
ujenzi wa barabara ya Mbinga – Mbamba bay kwa kiwango cha lami yenye
urefu wa Kilomita 66 unaofanywa na Kampuni kutoka China ya CHICCO,
Januari 5, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu wa Jimbo la Mbinga,
John Ndimbo wakati alipowasili kwenye kijiji cha Nyoni wilayani Mbinga
kuhutubia mkutano wa hadhara Januari 4, 2019. Kulia ni Sheikh wa wilaya
ya Mbinga, Said Majid.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimina na Mbunge wa Nyasa na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya wakati alipokagua ujenzi wa barabara ya Mbinga- Mbamba bay kwa kiwango cha lami yenye urefu wa Kilomita 66, Januari 4, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...