WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa jana Desemba 31, 2018 alizindua tawi la benki ya
CRDB wilayani Ruangwa pamoja na kupokea madarasa mawili yaliyojengwa
katika Shule ya Sekondari ya Kassim Majaliwa
kwa udhamini wa Benki ya CRDB, iliyopo katika Kijiji cha Kilimahewa.
Waziri
Mkuu aliushukuru uongozi wa benki hiyo kwa kufanikisha kujenga tawi
hilo ambalo litahamasisha ukuaji wa uchumi pamoja na kuwawezesha
wananchi wa Ruangwa kujua umuhimu wa kuhifadhi fedha zao benki.
Kadhalika,
Waziri Mkuu alisema ni vema kwa benki ya CRDB ikasogeza huduma hususan
kwa wananchi waishio katika miji mikubwa iliyo mbali na makao makuu ya
wilaya kwa kufungua ofisi za uwakala na kuwaondolea adha ya kutembea
umbali mrefu.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Tawi la
Benki ya CRDB wilayani Ruangwa Mkoani Lindi, Desemba 31, 2018. Wengine
pichani ni kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilwa,
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Laay, Meneja wa Benki ya CRDB
Tawi la Ruangwa, Method Muganyizi, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB,
Abdulmajid Nsekela pamoja na Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (wa tatu kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Laay wakifungua pazia katika kibao kuashiria ufunguzi rasmi wa Tawi la Benki ya CRDB wilayani Ruangwa Mkoani Lindi, Desemba 31, 2018. Wengine pichani ni kutoka kulia ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama
Mary Majaliwa, Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela pamoja na Meneja wa
Benki ya CRDB Tawi la Ruangwa, Method Muganyizi.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuashiria uzinduzi wa madarasa
mawili katika Shule ya Sekondari ya Kassim Majaliwa yaliyojengwa na
Benki ya CRDB, iliyopo katika Kijiji cha Kilimahewa, Ruangwa mkoani
Lindi Desemba 31, 2018. Wengine pichani kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya
ya Ruangwa, Hashim
Mgandilwa, Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Laay,
Mke wa Waziri Mkuu, Mama
Mary Majaliwa, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka
pamoja na Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki
hiyo, Tully Esther Mwambapa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Laay, Mke wa Waziri Mkuu, Mama
Mary Majaliwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakiwa wameketi katika madeski pamoja
na baadhi ya wanafunzi katika moja ya madarasa hayo yaliyojengwa na
Benki ya CRDB.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...