KOCHA Mkuu wa timu ya Yanga Zahera Mwinyi amemteua mshambuliaji wa timu hiyo Ibrahim Ajib kuwa nahodha akichukua nafasi ya beki kisiki Kelvin Yondani.
Hatua hiyo imekuja baada ya Yondani kuchelewa kuripoti mazoezini bila kutoa taarifa yoyote na kuonesha utovu wa nidhamu akiwa kama kiongozi uwanjani.
Zahera amechukua hatua hiyo baada ya Yondani kutoonekana mazoezini licha ya wenzake wote kuanza mazoezi.
“Haiwezekani unatoa siku tano za mapumziko, mtu hatokei na hakuna taarifa yoyote. Sipendi hii tabia nimemtoa Yondani, nahodha mpya sasa atakuwa ni Ibrahim Ajibu,” alisema.
“Haiwezekani unatoa siku tano za mapumziko, mtu hatokei na hakuna taarifa yoyote. Sipendi hii tabia nimemtoa Yondani, nahodha mpya sasa atakuwa ni Ibrahim Ajibu,” alisema.
Ajibu anakuwa nahodha wa Yanga kwa mara ya kwanza baada ya kupendekezwa leo hii na Kocha wa timu hiyo Zahera akiamua kumng’oa Yondani kwa madai ya utovu wa nidhamu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...