![]() |
Sekretarieti ya Shirika la Kuzuia Silaha za
Kemikali (Secretariat of the Organization for the Prohibition of Chemical Weapons- OPCW) imetangaza
nafasi za kazi za Afisa Mwandamizi wa Masuala ya Umma na Afisa wa Masuala ya
Umma (Public Affairs Officer P-4 and Public Affairs Officer P-2).
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
inawahimiza Watanzania, hususan wanawake kuchangamkia nafasi hizo ambapo mwisho
wa kufanya maombi kwa nafasi ya Public
Affairs Officer P-4 ni tarehe 24 Januari 2019 na ile ya Public Affairs Officer P-2 ni tarehe 9
Januari 2019.
Maombi yafanywe kwa njia ya mtandao kupitia tovuti www.opcw.org ambayo pia ina maelezo zaidi kuhusu nafasi hizo.
Imetolewa
na:
Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki,
Dodoma.
4 Januari
2019
|
Home
Unlabelled
Tangazo la Nafasi za Kazi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...