Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
ABIRIA na wafanyabiashara ndogondogo katika kituo cha daladala cha Mbezi mwisho jijini Dar es salaam wamelalamikia gharama kubwa ya choo cha umma kilichopo kituoni hapo, huku wakisema kuwa gharama hiyo  imekuwa tofauti na vituo vingi vya daladala.

Wakizungumza na globu ya jamii kwa nyakati tofauti baadhi ya abiria na wafanyabiashara kituoni hapo wamesema kuwa malipo ya shilingi 500 kwa kulipia huduma ya choo ni kubwa sana ukilinganisha na sehemu nyingi ambazo bei yake ni shilingi 200 na wameomba mamlaka inayosimamia huduma hiyo kuiangalia kwa mara ya pili hasa kwa kupunguza gharama.

Kwa upande wao madereva na makondakta wa daladala wamesema kuwa wanalazimika kutumia mifuko ya plastiki au chupa za maji kama vyoo na hiyo yote ni kuepuka gharama hiyo.

"Tunakaa hapa kituoni muda mwingi kwa siku unaweza kutumia hata shilingi 5000 kwenda chooni tuu, ni bora tutumie tuu chupa ili kuokoa gharama" ameeleza mmoja wa dereva anayefanya safari zake kutoka Mbezi hadi Makumbusho.

Hadi Globu ya jamii inaondoka eneo la tukio haikufanikiwa kuwapata wahusika wa huduma hiyo kituoni hapo jitihada za kuwapata zinaendelea.
 Muonekano wa bei za huduma ya choo katika kituo cha mabasi Makumbusho jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa bei za huduma ya choo katika kituo cha mabasi Mbezi mwisho jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka, Blogu ya jamii)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...