Na Khadija Seif, Globu ya Jamii
MWANAMUZIKI wa miondoko ya Bongofleva Godfrey Tumaini a.k.a ‘Dudu Baya' anashikiliwa na jeshi la polisi katika kituo cha Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Michuzi Blog Kamanda wa polisi Kinondoni, Mussa Taibu ameweka wazi kwa sasa Dudubaya anashikiliwa kwa mahojiano.
Akizungumza na Michuzi Blog Kamanda wa polisi Kinondoni, Mussa Taibu ameweka wazi kwa sasa Dudubaya anashikiliwa kwa mahojiano.
Hii ni kufatia agizo alilolitoa jana Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kwa jeshi la polisi kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa (BASATA) kuhakikisha linamchukulia hatua kali Dudu Baya.
Pia Mwakyembe aliweka wazi sababu za kumchukulia hatua mwanamuziki huyo kutokana na makosa ya kumkashifu, aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji (Clouds Media Group) Marehemu Ruge Mutahaba.
Baada ya amri hiyo, Basata na jeshi la polisi limemfikisha Dudu Baya kituo cha polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam. Sanjari na hilo Mwanamuziki huyo anakabiliwa na Makosa ya matumizi mabaya ya mtandao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...