Naibu Gavana wa BoT Dk.Benard Kibese akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa  Malipo ya Papo kwa Papo Tanzania Instant Payment System (TIPS) katika ukumbimwa mikutano wa benki hiyo jana.
  Benald Jeremia Dadi Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Taifa Ndani ya Benki Kuu wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa  Malipo ya Papo kwa Papo Tanzania Instant Payment System (TIPS)
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bw. Abdulmajid Nsekela akitoa ujumbe wake kutoka muungano wa mabenki Tanzania TBA katika uzinduzi huo.
 Sosthenes Kewe Mkurugenzi wa Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania naye akitoa neno katika uzinduzi huo. Sosthenes Kewe Mkurugenzi wa Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania naye akitoa neno katika uzinduzi huo.





Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

BENKI Kuu (BoT) imezindua Mfumo wa Malipo ya Papo kwa Papo Tanzania(TIPS) wenye lengo la kurahisha kufanya malipo mbalimbali ya miamala ya fedha kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa uhakika na salama zaidi.

Uzinduzi huo umefanyika Benki Kuu ya Tanzania(BoT) jijini Dar es Salaam ambapo  viongozi wa ngazi mbalimbali kutoka taasisi za fedha na serikalini wamehudhuria huku Naibu Gavana wa BoT Dk.Benard Kibese akitumia uzinduzi huo kufafanua umuhimu wa mfumo huo kwa kina.

Akizungumza zaidi wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo wa Taifa ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bernard Dadi amesema Mfumo wa Malipo ya Papo kwa Papo Tanzania(Tanzania Instant Payment System) utamuwezesha utumaji wa fedha toka taasisi moja kwenda nyingine kufanya malipo bila kutumia fedha za kampuni nyingine.

"Kwa hiyo tutakuwa mfumo pale BOT ambao sasa mteja wa kampuni moja kwa mfano Vodacom anaweza kutuma fedha kwenda kwenye benki yoyote ile bila gharama. Kwa mfumo huu tutakuwa na majina sehemu moja kwa hiyo ukituma fedha ule muamala ambao umetumwa hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi wa jipa kwani kupitia mfumo huu utachukua jina kamili na kutuma kwa mteja tena kwa usalama kwani jina na fedha zitakuwa zimehakikiwa.

"Mfumo huu tunatarajia utajengwa ndani ya miezi 18 kupitia watalaamu wetu wa ndani ya BoT pamoja na wataalam wa taasisi nyingine za fedha na baada ya hapo sasa tutakwenda ndani zaidi kwa kuhakikisha tunamhudumia mteja wa kijijini kwa haraka na uhakika zaidi.Hivyo kupitia mfumo huu tunaamini sasa huduma za kufanya malipo ya fedha uko salama zaidi,"amesema.

Amefafanua sababu za kuiita mfumo huo ni Instant maana yake ni kwamba ndani ya sekunde moja hadi mbili fedha itakuwa imemfikia mteja tena ikiwa kamili bila kukosewa wakati kabla ya mfumo huo wapo ambao wamekuwa wakilalamika fedha kwenda kwa watu ambao si walengwa kutokana na kukosewa kwa jina au namba iliyokusudiwa.

Dadi ameongeza kuwa mfumo huo wanaamini utaleta ufanisi zaidi katika utumaji wa fedha, pia utaleta udhibiti na kwamba badala ya kwenda kuomba taarifa kwenye kampuni sasa hizo taarifa zitapatikana BoT."Kwa kutumia mfumo huu BoT tutakuwa tunajua miamala ambayo inafanyika kwa kila mwezi,hivyo hata Serikali itapata kodi stahiki kutokana na huduma hizo za malipo ya fedha."

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Kuendeleza  Sekta ya Fedha Tanzania Sosthenes Kewe  amesema mfumo huo ambao maandalizi yake umezinduliwa leo unathamani kubwa kwa maisha ya watu kwani utakapoanza kufanya kazi utapunguza gharama za utumaji wa fedha na kutoa taarifa mbalimbali za wanaotumia huduma za fedha kwa kufanya miamala mbalimbali

Amesema inafahamika katika maisha ya mtu ya kila siku watu wanafanya miamala mingi sana na kwa kutumia fedha tasilimu ambapo gharama yake inakuwa kubwa lakini kupitia mfumo huo sasa utarahisisha muda na gharama."Kwa sasa mtu akitaka kufanya malipo atalazimika kwenda benki ambapo ili afanye kwa haraka atachukua na bodaboda ambayo nayo ni gharama lakini mfumo huu malipo yatafanyika kwa urahisi na haraka bila kusababisha gharama yoyote."

Pia amesema mfumo huo utasaidia wakulima kulipa au kupokea fedha kirahisi, wafanyabiashara wataweza nao kufanya malipo ya miamala mbalimbali na kubwa zaidi utasaidia kupunguza adha kwa watu mbalimbali katika kufanya miamala na kwamba hata Serikali itakuwa na urahisi wa kulipa fedha katika taasisi mbalimbali.

"Tuone kwamba hii ni bahati ya pekee kwa watanzania kuwa na mfumo kama huo na tunawaomba wadau wote washiriki kikamilifu katika kuandaa mfumo huo ambao una tija kubwa kwa Watanzania wote nchini,"amesisitiza.

Wakati huo huo Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki ya CRDB ambaye pia ni Mwenyekiti wa Muungano wa Mabenki Tanzania Abdulmajid Nsekela amesema mfumo huo ni ubunifu ambao umesubiriwa kwa muda mrefu, hivyo kuzinduliwa kwake utasaidia benki zote nchini kutoa huduma mbalimbali za fedha kwa haraka na wakati.

"Pia mfumo huu utasadia benki nyingi kujitawanya maeneo mengi ya nchi yetu kwa gharama nafuu kwani kujenga tawi moja gharama yake ni kubwa lakini sasa kupitia mfumo huu benki zitaendelea kutoa huduma kwa wateja wao kwa urahisi zaidi.Lakini kikubwa zaidi utapunguza matumizi ya fedha tasilimu ambalo limekuwa tatizo kubwa kwa wananchi wengi, hivi sasa ukitaka kufanya malipo mbalimbali utatumia mfumo huu na hivyo utaondoa usumbufu.Tunawapongeza Benki Kuu kutokana na kuja na mfumo huu ambao pia unafanya taarifa nyingi zinakuwa sehemu moja.

"Kwa sasa ukienda mtaani utakutana na mawakala wengi na mmoja anahudumia karibu kampuni tano za mitandao ya simu anapotaka kufanya muamala kwa ajili ya mteja wake.Sasa mfumo huu wakala hana sababu ya kusumbuka kwa kuwa na kampuni nyingi kwani mfumo utamuwezesha kutumia sehemu moja kufanya aina yoyote ya miamala.CRDB tunapongeza ubunifu wa aina hii wenye lengo la kuboresha sekta ya huduma za fedha,"amesisitiza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...