Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akishangilia ushindi wa
timu ya mpira wa pete baada ya timu hiyo kuifunga timu ya pete ya
Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila magoli 17-1 katika mchezo wa
Bonanza uliofanyika katika Viwanja vya Jakaya Kikwete Youth Park
(Kidongo Chekundu) jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni
wakurugenzi na watumishi wa hospitali hizo wakishangilia pamoja.
Kepteni wa timu ya mpira wa miguu
wa Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila akishangilia baada ya
kuifunga timu ya Muhimbili ,Upanga bao moja kwa sifuri. Muhimbili
Mloganzila 1-0 Muhimbili Upanga. Wengine katika picha hii ni Wakurugenzi
wa Muhimbili Upanga na Muhimbili Mloganzila.
Mashabiki wa timu ya mpira wa
miguu ya Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila wakishangilia pamoja
baada ya timu yao kuifunga timu ya Muhimbili Upanga bao 1-0.
Mashabiki wa mpira wa miguu wakifuatilia mechi kati ya timu ya Muhimbili Upanga na Muhimbili-Mloganzila.
Mechi ikiendelea katika viwanja vya Jakaya Kikwete Youth Park (Kidongo Chekundu) leo.
Wachezaji wa mpira wa pete wa
Muhimbili Upanga wakiifungia timu yao bao la sita katika mchezo
uliofanyika Jakaya Kikwete Youth Park (Kidongo Chekundu). Muhimbili
Upanga 17- 1 Muhimbili-Mloganzila.
Baadhi ya mashabiki wakifuatilia
mpira wa pete uliofanyika leo kwenye viwanya vya Jakaya Kikwete Youth
Park (Kidongo Chekundu).
Baadhi ya watumishi wa Muhimbili wakifanya mazoezi ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo wa mpira wa pete na mpira wa miguu.
Wachezaji wa Muhimbili Upanga na Muhimbili-Mloganzila wakiwa katika picha ya pamoja.
…………………………………………………………………………
Bonanza
la michezo lililoandaliwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
limefana na kuleta ushindani mkubwa kwa timu shiriki za mpira wa pete na
miguu za hospitali hiyo na hivyo timu hizo kugawana makombe.
Bonanza
hilo limehusisha timu za Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)-Upanga
pamoja na Hospitali Taifa Muhimbili-Mloganzila ambapo katika mchezo wa
mpira wa Pete Muhimbili-Upanga imeichapa Muhimbili-Mloganzila magoli 17
kwa 1.
Katika
mchezo huo timu ya Mloganzila ilionekana kuelemewa kwani walipokua
wakifika langoni mwa timu pinzani walishindwa kufunga na hivyo kuwapa
uhakika wa kushinda mabao mengi.
Kwa
upande wa mpira wa miguu katika kipindi cha kwanza dakika ya 14 timu
ya Muhimbili Mloganzila imeichabanga bao 1 kwa 0 timu ya Muhimbili
Upanga bao lililofungwa na mshambuliaji machachari Edger Mtitu. Katika
kipindi hicho cha kwanza timu ya Muhimbili Mloganzila ilitawala mpira
na kusababisha Muhimbili Upanga kushindwa kufurukuta uwanjani.
Baada
ya kumalizika kwa mchuano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili Prof.
Lawrence Museru alizungumzia umuhimu wa kuendeleza michezo mahala pa
kazi ili kudumisha amani, umoja na upendo na pia watumishi kuwa na afya
bora hatua ambayo italeta tija katika maeneo ya kazi.
“Nitaendelea
kuunga mkono suala la michezo na kusapoti kadiri inavyowezekana maana
michezo ni afya, hivyo nawasihi watumishi wa Hospitali ya Muhimbili
Upanga na Mloganzila kuendeleza michezo na mjitokeze kwa wingi kushiriki
katika michezo mbalimbali,”amesema Prof. Museru.
Kwa
upande wao washiriki wa Bonanza hilo wameushukuru uongozi wa hospitali
kwa kufanikisha shughuli hiyo ambayo imewaweka karibu watumishi wote wa
MNH Upanga na Mloganzila.
Bonanza
la michezo la Hospitali ya Taifa Muhimbili, Upanga na Mloganzila
limefanyika katika viwanja vya michezo vya Jakaya Kikwete Youth Park
Kidongo Chekundu jijini Dar es salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...