Na. Atley Kuni- Dodoma
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia masuala ya Afya Dkt. Dorothy Gwajima, amewaonya na kuwatahadharisha watendaji katika ofisi hiyo kuepuka ubinafsi na kuwahimiza kufanya kazi kwa pamoja. Dkt.Gwajima ametoa kauli hiyo jijini Dodoma, wakati wa kikao kazi kilicho wakutanisha Wakurugenzi, wakurugenzi wasaidizi na Maafisa wa Wizara hiyo kutoka Idara za TEHAMA pamoja na Afya, wkati wa wasilisho la mfumo wa uendeshaji wa shughuli za Serikali (GoTHOMIS).

 Alisema,iliwaweze kufanikiwa lazima wafanye kazi kama timu moja bila kubaguana na kuonya, tabia ya ubinafsi sio nzuri na kama wanataka kukwama katika mipango yao watangulize ubinafsi mbele badala ya maslahi ya nchi kwanza. “Mimi sipo tayari kuona tunakwama wakati nilikula kiapo mbele ya Mhe. Rais, ni bora mniondoe lakini nitasimama katika kweli .“alisema Gwajima.

 Dkt.Gwajima alisema anashangazwa na mataifa ya Ulaya kuendelea kupiga hatua kwenye maendeleo huku Watanzania tukibaki nyuma. “Lakini kikubwa ninacho kiona ni hali ya uratibu (Cordination) ndio changamoto kubwa katika utendaji wetu wa kila siku.” alibainisha Dkt.Gwajima.

Naibu Katibu Mkuu huyo, amezitaka Idara hizo kushirikiana kwa karibu hasa ikizingatiwa mabadiliko ya sasa ya sayansi na teknolojia yanahitaji uwajibikaji wa pamoja. “Natambua tunafanya kazi nzuri sana, lakini bila kuishirikisha kwa karibu idara ya TEHAMA, hatutaweza kufika tunapotaka kwenda” alisema Gwajima.

Kwa upande wake Mkurugenzi msaidizi kutoka Idara ya Afya wizarani hapo, Dkt. Anastazia Nswila, aliwataka wajumbe kuwa na msimamo  mmoja katika maamuzi, kuacha kutegemea na kupangiwa misaada mbalimbali kutoka kwa wadau . “Wadau wana pesa nyingi, isiwe sababu yakutupangia nini watatuletea, ni vizuri mahitaji yatoke kwetu sisi, kama ni Laptop tuwaambie ni aina gani tunataka, kama ni vifaa tiba huko kwenye kwenye vituo sisi ndio wakuamua aina gani ya vifaa vinafaa kulinga na mazingira yetu” alisisitiza Dkt. Nswila.

Kikao hicho kilichodumu kwa takribani saa 3 kimetoka na maazimio matano ikiwepo, kuandaliwa mafunzo maalumu kwaajili yakuwawezesha idara mama ya masuala ya afya kuutambua mfumo, kuandaa andiko la jinsi gani Wizara hiyo inavyofanya katika mfumo huo, kila Wizara ifanye maamuzi ya kisekta ya ndani kabla yakukutana TAMISEMI na Wizara ya Afya, na mwisho kuwa na kikao cha wadau ili kuwapa muelekeo na msimamo wa Serikali.
 Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI (Afya), Dkt. Dorothy Gwajima alipokuwa akiongea na watendaji hao wa Wizara wakati wa kikao cha kupitia mifumo ya Afya kwenye ukumbi wa Reform mkoani Dodoma.
 Moja ya Wakurugenzi, Dkt. Anna Nswila, akichangia mada wakati wa kikao cha kupitia mifumo ya Afya kwenye ukumbi wa Reform mkoani Dodoma.
Mmoja ya maafisa wa Wizara hiyo, aliposimama kushauri jambo wakati wa kikao cha kupitia mifumo ya Afya kwenye ukumbi wa Reform mkoani Dodoma.
 Baadhi ya wakurugenzi, Wakurugenzi wasaidizi na maofisa wengine wa Wizara hiyo, wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Dkr. Dorothy Gwajima wakati wa kikao cha kupitia mifumo ya Afya kwenye ukumbi wa Reform mkoani Dodoma.
  Naibu katibu Mkuu na Timu ya (RHMT) ya Mkoa wa Dodoma alipofanya ziara yake ya kwanza na kuhimiza uwajibikaji na uratibu wa kazi kwa pamoja wakati wa ziara yake ya kwanza toka aingia katika Wizara hiyo aliyoifanya kwenye Sekretarieti ya mkoa wa Dodoma. (Picha na habari na Atley Kuni-OR-TAMISEMI)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...